BILIONI SITA KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI YA MANISPAA MOSHI, BILIONI 44 VIFAA TIBA


Na WAF - Moshi, Kilimanjaro 


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha zaidi ya Bilioni 44 kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa Tiba pamoja na Bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Manispaa Moshi ambapo Hospitali hiyo ikikamilika itakua imegharimu Shilingi Bilioni Sita.  

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo leo Oktoba 6, 2024 baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Moshi pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Kata ya Mabogini ikiwa ni siku ya Tatu ya ziara yake katika Mkoa wa Kilimanjaro. 

"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kujali Watanzania, na sasa ametoa shilingi Bilioni 44 kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa Tiba vitakavyotumika katika Hospitali ya Manispaa Moshi ikikamilika, lakini pia ametoa Bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hii unaoendelea na ikikamilika itatumia Bilioni Sita." Amesema Waziri Mhagama

Aidha, Waziri Mhagama ameonesha utofauti wa fedha zilizotolewa katika kipindi kilichopita na kipindi cha sasa ambapo kwa kipindi hiki fedha zimetolewa nyingi zaidi lengo likiwa ni kuboresha miundombinu ya utolewaji wa huduma za Afya nchini. 

"Katika Mkoa wa Kilimanjro kwa kipindi kilichopita ulipokea Bilioni Nane kwaajili ya Vifaa Tiba lakini kwa kipindi hiki kifupi chini ua uongozi mahiri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Shilingi Bilioni 44 kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa Tiba ikiwemo X-Ray, Ct-Scan, vitanda vya wagonjwa, vitanda vya kujifungulia pamoja na dawa." Amesema Waziri Mhagama

Waziri Mhagama akiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Kata ya Mabogini amewaeleza wananchi kuwa Serikali imeleta fedha kwaajili ya miradi mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya ambapo fedha zilizoletwa ni kiasi cha shilingi Bilion 129 zitakazoshughulikia Sekta ya Afya katika Halmashauri hiyo. 

Amesema, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Kata ya Mabogini ikikamilika itakua na wodi za kulaza wagonjwa pamoja na nyumba za watumishi ili wananchi wasipate tabu pindi wanapataka kupata huduma za afya hata ikiwa ni usiku. 

"Kwakweli tuna kila sababu ya kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mwenye maono na uongozi wake bora wa kujali za wananchi, maendeleo haya ambayo yamefanywa kwenye Manispaa hii na mkoa mzima wa Kilimanjaro ni makubwa na hayajawahi kutokea." Amesema Waziri Mhagama











Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

ZAIDI YA BILIONI 23 KUTUMIKA KUSAMBAZA UMEME KILIMANJARO VIJIJINI

✔️VIJIJI 506 VIMEUNGANISHWA NA UMEME KATI YA VIJIJI 519 SAWA NA 97.49%


Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 23.7 ili kuhakikisha miradi yote ya kusambaza umeme vijijini Mkoani Kilimanjaro inakamilika na kuwapatia wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii

Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amebainisha hayo mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Nzowa Julai 29 Mkoani Kilimanjaro wakati wa utambulisho wa Wakandarasi walioshinda tenda ya kusambaza umeme katika vijiji 13 vilivyokuwa vimesalia. 

"Hadi sasa tumeunganisha umeme katika vijiji 506 kati ya vijiji 519 ambayo ni sawa na asilimia 97.49 Mkoani hapa; na leo hii tupo hapa kutambulisha Wakandarasi watakaotekeleza miradi katika vijiji hivi vilivyosalia," amebainisha Mhandisi Olotu.

Mhandisi Olutu amebainisha kuwa kwa Mkoa wa Kilimanjaro REA inatekeleza jumla ya miradi mikubwa mitatu ambayo ni mradi wa shilingi bilioni 13.1 wa kusambaza umeme vijijini, mradi wa bilioni 8.8 wa kusambaza umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo na mradi wa bilioni 1. 7 wa kusambaza umeme katika vituo vya afya na visima vya maji. 

"Tumefika hapa kwa lengo la kutambulisha Wakandarasi watakokamilisha kazi iliyobaki Mkoani hapa sambamba na kutambulisha wasimamizi wake kwa upande wa REA ambao miongoni mwa majukumu walionayo ni kuwasilisha kwako taarifa za mara kwa mara za maendedeleo na hatua za utekelezaji," amefafanua Mhandisi Olotu. 

Akizungumza wakati wa utambulisho wa wakandarasi hao; Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Nzowa ameipongeza REA kwa kuendelea kufanikisha dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo wananchi wake kupitia umeme. 

"Umeme ni injini ya uchumi wa taifa lolote duniani na kwakutambua hilo, Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza fedha nyingi katika Sekta ya Nishati na kwa bahati nzuri REA mmetambua vyema dhamira ya Mhe. Rais na mnatekeleza kwa vitendo," amepongeza Nzowa. 

Aidha, amewataka Wakandarasi waliopewa jukumu hilo la kufikisha umeme katika vijiji vilivyosalia kufanya kazi kwa weledi na kwa kasi ili kukamilisha na kukabidhi mradi ndani ya muda uliopangwa. 

"Wote mliopewa jukumu ni wazawa; hatutarajii kuona kazi ikikwama; kukitokea changamoto yoyote Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ipo wazi kuwasikiliza na kusonga mbele," amesisitiza Nzowa. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Wakandarasi hao waliahidi kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na kasi ili kutimiza dhamira ya Serikali. 

"Serikali imetuamini kwa kutupa kazi, nasi tunaahidi kuhakikisha hatufanyi makosa; tutatekeleza kazi hii kwa uzalendo ili sote kwa pamoja tutimize dhamira ya Rais wetu," amesema Mhandisi Cuthbert Shirima, Mkandarasi kutoka Kampuni ya Transpower Limited. 

Kampuni zilizopewa jukumu la kukamilisha vijiji 13 vilivyosalia Mkoani humo ni Northern Engineering works Ltd (Wilaya ya Hai), Radi Services Ltd (Wilaya ya Hai na Moshi), Transpower Ltd (Wilaya ya Same) na Octupus Engineering Ltd (Wilaya ya Mwanga).



 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa