Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Mosi (MoCU) Prof ,Faustine Bee
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Upimaji wa Homa ya Ini kwa Watumishi
wa Chuo hicho pamoja na Wategemezi wao, zoezi ambalo linafanyika katika
kituo cha Afya kilichopo chuoni hapo .
Baadhi
ya Wauguzi wanaohudumu katika kituo hicho fcha Afya pamoja na Watumishi
wa Chuo hicho wakifuatilia hotupa ya Uzinduzi wa zoezi la Upimaji wa
Homa ya Ini iliyotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi
(MoCU)
Mganga
Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU)
,Eustace Ng'weshemi akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji
wa Homa ya Ini katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi .
Baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi ,wakiwa katika uzinduzi huo.
Mganga
Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU)
Dkt , Eustace Ngw'eshemi akimuonesha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Ushirika ,Moshi ,Prof Faustine Bee namba ya siri itakayotumika wakati wa
kupokea majibu baada ya zoezi la upimaji kukamilika.
Mkuu
wa kitengo cha Maabara katika Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha
Ushirika (MOCU) Aniseth Malenga akivuta Damu katika mkono wa Makamu Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Prof Faustine Bee alipoongoza zoezi la
upimaji wa Homa ya Ini kwa watumishi wa chuo hicho.
Mkuu
wa Kitengo cha Maabara katika kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha
Ushirika (MoCU) Aniseth Malenga akivuta Damu katika mkono wa Mmmoja wa
watusmihi katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Julieti Bee wakati wa uzinduzi
wa zoezi la upimaji wa Homa ya Ini chuoni hapo.
Mganga
Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU)
Dkt , Eustace Ngw'eshemi akizungumza na mmoja wa watumishi wa Chuo Kikuu
cha Ushirika Moshi kabla ya kumfanyia vipimo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
CHUO
kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) kimezundua zoezi la upimaji wa Homa ya
Ini kwa Watumishi ,Wategemezi wao pamoja na majirani wa cuo hicho ikiwa
ni njia ya tahadhari licha ya kutokuwepo ushahidi wa mlipuko wa ugonjwa
huo nchini.
Serikali
inatambua umuhimu wa afya bora kwa watumishi wake kwani afya bora ni
rasilimali muhimu kwa maendeleo na maenedeleo ya Taifa yataletwa na
wananchi pamoja na watumishi wenye Afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali
na kutoa huduma stahiki kwa umma wa Tanzania.
Katika
kuzingatia sera na miongozo ya Afya ya mwaka 1990 iliyopitiwa mwaka
2007 ,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) kama mdau imeanza kutoa
huduma ya upimaji wa Ini kupitia Kituo chake cha Afya kilichopo chuoni
hapo.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) Prof Faustine Bee akatumia
zinduzi huo kutoa wito kwa watu wengine waishio nje ya mazingira ya Chuo
hicho kutumia kituo hicho pindi wanapohitaji huduma za matibabu.
Zaidi
ya watumishi 456 wanashiriki katika zoezi la Upimaji wa Ini chuoni hapo
huku Menejimenti ikiwa katika mazungumzo na Hospitali ya Rufaa ya KCMC
ukiona uwezekano wa Wagonjwa wanaohitaji rufaa kwenda moja kwa moja KCMC
badala ya kupitia Hosptali ya Mkoa ya Mawenzi kama ilivyo sasa.
0 comments:
Post a Comment