VIJANA
wajasiriamali wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamefanikiwa kujinyanyua
kiuchumi kwa kukusanya sh40 milioni, kupitia kikundi cha kuweka na
kukopa (SACCOS) waliyoianzisha kwa vikundi 68 kujiunga nayo, kati ya
vikundi 97 vya ujasiriamali vilivyosajiwa.
Kati
ya vikundi hivyo 68, vilivyojiunga na SACCOS, hadi sasa vikundi 12
vimepata mikopo, ambapo kila kikundi kina wanachama 30 sawa na watu 360
wameanza kunufaika kupitia sh40 milioni kwenye mikopo wanayokopeshana.
Katibu
wa UVCCM wilayani Simanjiro, Bakari Mwacha aliyasema hayo wakati
akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Mwenyekiti wa UVCCM wa mkoa wa
Manyara Mosses Komba alipofanya ziara ya siku moja. Mwacha
alisema kupitia SACCOS hiyo vijana hao wanachukua mikopo na kurudisha
kwa wakati na uaminifu kupitia shughuli za ujasiriamali wanazozifanya.
Alisema
wanatoa ombi kwa halmashauri ya wilaya hiyo kutoa kipaumbele kwa vijana
hao kuwapatia ile mikopo ya asilimia 5 ya mapato ya ndani kwani
wataweza kuirejesha kwa wakati tofauti na vijana wengine. "Hawa
wana uzoefu hata wakipewa mikopo inakuwa kwenye mikono salama tofauti
na wengine ambao wakipewa wanasuasua kurejesha ila vijana wetu watakuwa
na uhakika kwani wana SACCOS yao," alisema Mwacha
Alisema
vijana wengi wanajiunga na uanachama kwenye jumuiya hiyo ambapo hadi
sasa wapo 9,205 na wengine wapya 139 wamejiunga mji mdogo wa Mirerani. Mwenyekiti
wa UVCCM Mkoa wa Manyara, Mosses Komba aliupongeza uongozi wa UVCCM
wilaya ya Simanjiro, kwa kusimamia ipasavyo vikundi hivyo hadi
kupatikana kwa fedha hizo na kujinufaisha kiuchumi.
"Mmekuwa
mfano bora kwa vijana wa mkoa wa Manyara, kwani wilaya nyingine
zinapaswa kuiga mfano wenu wa kuchangamkia fursa za kuongeza kipato,"
alisema Komba. Alisema
baada ya kuwa na vikundi hivyo suala la kupatiwa mikopo na halmashauri
ya wilaya ya Simanjiro, litakuwa rahisi kwani ninyi mtakuwa na uzoefu wa
kufanya ujasiriamali.
Mwenyekiti
wa UVCCM wa wilaya ya Simanjiro, Thomas Mollel alisema atahakikisha
anapigania upatikanaji wa asilimia tano ya mikopo kwenye halmashauri ya
wilaya ili vijana wapate mikopo. Mollel
alisema vijana wa Simanjiro wanapaswa kushirikiana kwa pamoja ili
kujijenga kiuchumi na kujitolea nguvu kazi ili kutekeleza ilani ya CCM.
0 comments:
Post a Comment