Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo akiwa katika operesheni ya 
uteketezaji wa mashamba ya mirungi iliyofanyika kuanzia tarehe 19
 hadi 25 Machi wilayani Same, Kilimanjaro.

***
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),
 kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, imefanya operesheni
 maalum wilayani Same, mkoani Kilimanjaro 
kuanzia tarehe 19 hadi 25 Machi 2025. Katika operesheni hiyo, 
ekari 285.5 za mashamba ya mirungi zimeteketezwa na
 watuhumiwa saba (7) wamekamatwa, akiwemo kinara wa biashara
 haramu ya mirungi nchini aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu,
 Interindwa Zinywangwa Kirumbi, maarufu kwa jina la mama Dangote.