
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Kanda (KCMC) kwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la huduma za tiba mionzi kwa matibabu ya wagonjwa wa saratani uliofunguliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.Mhe. Hasunga ametoa pongezi hizo leo baada ya Kamati ya Bunge ya PAC kufanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la huduma za tiba mionzi kwa matibabu ya wagonjwa wa saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda (KCMC) na kupokea taarifa ya ujenzi unaotarajiwa kukamilika Aprili 30, 2025."Kazi ya kamati...