Home » » ZIARA YA CHADEMA WILAYANI SAME JANA

ZIARA YA CHADEMA WILAYANI SAME JANA


Lema akiwasili Same.
Ally Banaga na James Ole Millya.
James Ole Millya akisalimiana na mwanachama wa CCM aliahamia CHADEMA Same jana.
John Heche - Same.

Katibu Mkuu wa TLP Same, Heriel Msolo(kulia) akirudisha kadi jana.

Vijana wakigombea ofa ya kadi 10 za Millya
Wananchi wa Same wakigombea foleni ya kupatiwa kadi za CHADEMA jana.
---
Na TUMAINIEL W. SERIA, ARUSHA.

CHADEMA wanaziara ya kichama Wilayani Same kwa siku nne, kuanzia jana hadi jumatatu chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana BAVICHA, Ngd Jhon Heche.

Wana mikutano maeneo tofauti ya Wilaya katika kuimarisha chama hicho.

Mkutano wa jana ulifanyikia viwanja vya Kwasakwasa Mjini Same kuanzia saa 9 hadi saa 12 jioni ambapo viongozi waliohudhuria ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mwenyekiti Bavicha, John Heche, Mweyekiti CHADEMA Kilimanjaro, Augustino Matemu na kiongozi wa vijana Babati, Wilson Mattaka.

Wengine ni James Ole Millya aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM Arusha, aliyekuwa Mjumbe wa NEC CCM kutoka Arusha, Ndg Ally Bananga na aliyekuwa Diwani wa Sombetion (CCM). Wote hawa walihamia CHADEMA mapema mwezi huu.

Katika mkutano huo kadi nyingi sana zilitolewa na kusainiwa na John Heche.. tena zikigombewa kununua. Lema litoa ofa ya kadi 10 kwa kina mama na Millya nae akatoa ofa ya kuwalipia vijana kumi.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa TLP Same, Ndg Heriel Msolo alirudisha kadi ya TLP na kupewa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa BAVICHA, John Heche.

Lema aliwataka watanzania kutokubali kugwanywa na wanasiasa kwa misingi ya udini na ukabila au ukanda na kueleza kwamba CHADEMA haipiganii maslahi ya kundi lolote katika hayo. Akasema hata yeye hapiganii maslahi yake binafsi bali ya watanzania.

John Heche aliwataka watanzania kujitokeza kutoa maoni yao kwa tume ya Katiba na kuelekeza kuwa wakatae au wazifanyie mabadiliko makubwa nafasi za uDC au uRC na nyinginezo za kuteuliwa na mtu mmoja. Akadai pia madaraka ya rais ni makubwa na mamabo mengi yameachwa kwa mtu mmoja. hali inayohitaji marekebisho ili kuwe na uwajibikaji wa pamoja.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa