Home » » MNAIGERIA AKAMATWA KIA

MNAIGERIA AKAMATWA KIA


Na Upendo Mosha, Moshi
MWANAMKE mmoja raia wa Nigeria, Vivian Edigni (38), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma zakukutwa na dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), akijiandaa kuelekea nchini Italia.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Robert Boaz alisema tukio hilo, lilitojkea juzi ambapo mwanamke huyo alikutwa na dawa aina ya Cocaine zilizofungwa kama pipi 15.

Alisema mtuhumiwa huyo, mwenye pasipoti yenye namba AO15290130 iliyotolewa nchini Nigeria, alikuwa akijiandaa kuelekea katika Jiji la Milani nchini Italia kupitia Addis Ababa, Ethiopia kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Alisema wakati wa upekuzi, mtuhumiwa alikutwa akiwa na pipi 15 katika mkoba wake wa mkononi.

"Kiasi hiki cha madawa ni kidogo kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara hizi, tulimtilia mashaka na tukamchukua tangu juzi mpaka jana, ameshatoa pipi nyingine 24 kwa njia ya haja kubwa,"alisema Kamanda Boaz.

Chanzo: Mtanzania


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa