Mwanga.
SERIKALI imesema inaanza kuchukua hatua dhidi ya watu wanaotumia
mwavuli wa dini kuleta vurugu zinazotishia amani na usalama wa nchi.
Makamu wa rais Dk. Mohamed Gharib Billal, amesema hayo leo wakati wa
kusherehekea sikukuu ya Eid el Hajji, ambayo kitaifa imeathimishwa
wilyani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Akihutubia baraza la Eid, katika masjidi ya Vuchama wilyani Mwanga,
Dk. Billal alisema hivi karibuni kumeibuka wimbi la watu
wanaojihusisha na vurugu za kidini ambazo chanzo chake kimekuwa ni
mgogoro miongoni mwa waumini wa dini.
Dk. Billal alisema kwa kiasi kikubwa vurugu hizo zimechafua sura y
taifa na kuleta taswira mbaya kwa jamii, kutokana na uvunjifu wa amani
na sheria za nchi unaofanywa na kikundi cha watu aliowaita wahuni.
Katika hatua nyingine Dk. Billal alisisitiza umuhimu wa taasisi za
dini kujiendesha kwa misingi ya kushauriana na kukubliana masuala
kadhaa ya kiutekelezaji na uendeshaji, ili kuepuka mifrakano
inayojitokeza hivi sasa miongoni mwa pande hizo.
Hata hivyo alisema serikali itaendelea kutimiza wajibu wake wa
kuhakikisa kwamba amani inalindwa ili iweze kuvisaidia vizazi vijavyo
na kuwa na nchi yenye uendelevu wa amani na utulivu.
Naye kaimu mufti wa Tanzania sheikh Ismail Habib Makusanya, wakati
akimkaribisha makamu wa rais kutoa hotuba yake aliiomba serikali
kuharakisha utafiti na uchunguzi utakaowezesha kubaini sababu za
kuvurugika kwa amani na utulivu uliopo.
Alisema kwa kiasi kikubwa migogoro inayojitokeza hivi sasa hususani
ile ya kidini ni tatizo linaloendelea kushika kasi hali inayopelekea
kuwepo uhraka wa kulitatua.
“Amani inaletwa na watu wakiwemo viongozi wa dini na serikali bila
kujali serikali hiyo ni ya Waislam au dini nyingine na serikali hii
sasa inatambua kuwa wajibu wake kuhakikisha kuwa amani inaendelea
kuwepo”, alisema.
Kaimu mufti alisisitiza serikali kutumia vyema vyombo vyake vya ulinzi
na usalama kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya wavunjifu wa amani
kwa haraka na kuchukua hatua zinazostahili kwa wale watakaobainika
kuhusika.
Wakati huo huo ameelezea tishio la aadhi ya wanasiasa wanaotumia
kivuli cha udini kuvuruga amani ya nchi na kutaka nao wachunguzwe na
kuchukuliwa hatua za kisheria kama raia wengine.
Sikukuu ya Eid el Hajji, imeambatana na uzinduzi wa wa msikiti wa
Vuchama pamoja na kuweka jiwe la msingi na uzinduzi wa mfuko wa
kujenga shule ya kituo cha Kiislam cha Vuchama.
Miradi hiyo inatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 4.4, ambapo makamu
wa rais Dk. Billal alichangia shilingi milioni tano, akifuatiwa na
viongozi wengine akiwemo waziri mkuu mstaafu Cleopa Msuya, aliyetoa
shilingi milioni moja, huku mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe
alichangia shilingi milioni moja.
0 comments:
Post a Comment