na Chalila Kibuda
MWENYEKITI
wa Baraza la Watoto Kata ya Kirangare, wilayani Same, Christopher Abduel,
amesema hali ya lishe kwa wototo katika kata hiyo, si nzuri kwani walazimika
kuishi kwa kula miwa.
Abduel
alibainsha hayo hivi karibuni wakati wa ziara ya waandishi kuangalia
utekelezaji wa mabaraza ya watoto wilayani Same.
Alisema
utaratibu wa wanafunzi kupewa chakula shuleni ulidumu kwa miezi kadhaa, kwani
baada ya hapo kulikuwa na ukame uliosababisha mazao kukauka hambani, hivyo
kuwalazimu watoto kushindia miwa.
Abduel
alisema kukosekana kwa chakula cha uhakika katika kata hiyo, ni moja ya sababu
za wanafunzi kushindwa kusoma kutokana na kukosa lishe sahihi ya kuweza
kufikiria shule.
“Watoto
wa Kirangare wamekuwa ndio wazalishaji katika familia hii ni changamoto ya
kuacha haki ya msingi ya kusoma na kuingia katika shughuli za uzalishaji mali,”
alisema Abduel.
Alisema
watoto wanatakiwa kupata chakula chenye virutubisho ambavyo vitawafanya kuwa na
akili ya kufanya vizuri, lakini kwa hali ilivyo sasa wanafikiria juu ya kupata
chakula na kuacha masomo.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment