Home » » WAHAMIAJI HARAMU 63 WATIWA MBARONI KILIMANJARO

WAHAMIAJI HARAMU 63 WATIWA MBARONI KILIMANJARO

Florah Temba,  Moshi.

WAHAMIAJI
 haramu 63 Raia wa nchini Ethiopia, wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro, kwa  tuhuma za kuingia nchini kinyume cha
sheria.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Koka Moita, alithibitisha kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu na kusema kuwa bado kumekuwepo na mtandao ambao unahusika na biashara ya kuwasafirisha watu hao.

Kulingana na taarifa ya kaimu kamanda Raia hao wa Ethopia,  waliingia nchini kinyemela kwa kupitia njia za panya,  bila ya kuwa na vibali vya kuwaruhusu kuingia nchini Tanzania.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu kamanda   alisema wahamiaji hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika wilaya ya Mwanga mkoani Hapa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na  kaimu kamanda,  Raia hao wa Ethiopia 53 walikamatwa April 10 majira ya saa moja kasoro robo  katika eneo la Miikocheni Kata ya Mwanga  huku  wengine 10 wakikamatwa April 11 majira ya saa sita usiku katika kata ya Kileo.

 “Wahamiaji hawa haramu 53 walikutwa wakiwa wamejificha kichakani katika eno la Mikocheni,lakini hao wengine 10  walikutwa wakiwa wanatembea tembea kama vile hawana mwelekeo wala hawajui pa kenda kkatika eneo la Kileo”alisema Kamanda.

Aidha kamanda alisema  wahamiaji hao walikamatwa na askari waliokuwa doroa katika maeneo hayo  na kwamba jeshi la polisi kwa  sasa wanaendelea na chunguzi ili kuubaini mtandao unaohusika na usafirishaji wa watu hao.

Alisema Raia hao wa nchini Ethiopia  wanashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi mjini Moshi na kwamba mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua za kisheria zitachukua mkondo wake

Hata hivyo kaimu kamanda aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kufanuikisha jitihada za kumaliza tatizo la wahamiaji haramu mkoani hapa. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa