Home » » KATIBU MKUU MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA MKOMAZI NA KUWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA WELEDI

KATIBU MKUU MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA MKOMAZI NA KUWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA WELEDI


Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alianza ziara yake Same kwa kufika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mwalimu Herman Kapufi kujitambulisha.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi na ujumbe wake wakipitia baadhi ya kurasa katika kitabu hicho.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa(aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi (suti nyeusi) eneo lenye mgogoro wa mpaka katika Hifadhi ya Mkomazi. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Malikale Donatius Kamambaa; Kaimu Mkurugenzi wa Mipango wa TANAPA Dk. Ezekiel Dembe na Mkurugenzi wa Utumishi Wizara ya Maliasili na Utalii Said Msambachi.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa akitoa Taarifa ya Hifadhi ya Mkomazi kwa Katibu Mkuu Maliasili na Utalii pamoja na ujumbe wake.
Watumishi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi wakiwa makini kumsikiliza Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alipowatembelea.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi (wa pili kulia) akizungumza na watumishi wa Hifadhi ya Mkomazi. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Malikale Donatius Kamamba, Mkuu wa Hifadhi ya Mkomazi Donat Mnyagatwa na Mkurugenzi wa Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Said Msambachi.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi katika picha ya pamoja na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akiangalia mbwa mwitu waliohifadhiwa katika uzio maalum kwa ajili ya kuwalinda Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
Picha zote na Pascal Shelutete.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa