Home »
» NAIBU MEYA KILIMANJARO AFARIKI DUNIA
NAIBU MEYA KILIMANJARO AFARIKI DUNIA
Naibu Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambaye pia ni
Diwani wa Kata ya Kiboriloni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Vincent Rimoy, amefariki dunia jana mchana.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Meya wa halmashauri hiyo,
Mstahiki Jaffari Michael, alisema Rimoy alifariki wakati akikimbizwa
hospitali baada ya kudondoka akiwa shambani kwake eneo la Mandaka, Mjini
Moshi.
"Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti
kwenye Hospitali ya Rufaa ya KCMC," alisema Mstahiki Michael pia ni
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Moshi Mjini.
Akizungumza na Majira,
mmoja wa wafanyakazi wa marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe
gazetini, alisema Rimoy aliamka asubuhi na kwenda shambani kwake baada
ya kutoka safari ya Dar es Salaam Novemba 4, mwaka huu (juzi).
Naye
mmoja wa rafiki zake na marehemu ambaye naye hakutaka jina lake
liandikwe gazetini, alisema kifo cha Rimoy kinaikumbusha familia yake
machungu yaliyowakuta miaka 23 iliyopita.
"Rimoy aliwahi kupata
ajali ya gari Sikukuu ya Pasaka mwaka 1990 akiwa na familia yake...
katika ajali hiyo alimpoteza mkewe na watoto wote watano, hakika
inasikitisha," alisema.
Mbali ya kuwa mwanasiasa, marehemu alikuwa
akijishughulisha na biashara akimiliki hoteli maarufu Mjini Moshi
inayoitwa New Castle, biashara ya ujenzi pamoja na kumiliki Shule ya St.
Patrick.
chanzo; majira
0 comments:
Post a Comment