Home » » Amuua jirani yake kwa rungu, panga

Amuua jirani yake kwa rungu, panga

VILIO na simanzi vilitawala katika Kijiji cha Kikavu Chini, Kata ya Machame Kusini wilayani Hai, baada ya Alex Peter kudaiwa kumshambulia jirani yake aliyefahamika kwa jina la Pili Mnyamvua (65) kwa kumpiga kwa rungu na panga hadi kusababisha kifo chake. Mashuhuda wa tukio hilo waliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa majirani hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu ambapo Pili alilalamikia mifugo (kuku) ya jirani yake kuingia shambani kwake na kula mazao mbalimbali.
Tukio hilo la kutisha lilitokea Desemba 7 mwaka huu, saa 8 mchana ambapo mtuhumiwa alikuwa kwenye shamba lake akiendelea na shughuli mbalimbali za kilimo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kikavu Chini, Swalehe Juma alisema kuwa baada ya tukio hilo kutokea wananchi walishikwa na hasira na kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa na kuchoma nyumba yake moto baada ya kuwatoroka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema hadi sasa hawajafanikiwa kumkamata mtuhumiwa.
“Taarifa hiyo tunayo ila mpaka sasa hatujaweza kumkamata mtuhumiwa ila bado Jeshi la Polisi linaendelea na jitihada zake ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa