Home » » ‘Tiba ya vurugu, maandamano nchini ni elimu kwa vijana’

‘Tiba ya vurugu, maandamano nchini ni elimu kwa vijana’

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Iddi Juma amesema tiba ya vurugu, migogoro na maandamano yasiyo ya lazima nikuhakikisha vijana wanapata elimu.
Akizungumza na RAI, Juma alisema uzoefu unaonyesha migogoro, vurugu na maandamano ambayo yamekuwa yakitokea nchini, washiriki wengi ni vijana hususan walewanaokaa vijiweni.

Juma alisema kwa mfano maandamanoyaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA Arusha, Mbeya na Dar es Salaam, vijana

wengi walitumika kwa vile hawana la kufanya hali inayochangiwa na kwa kiasi kikubwa na kukosa elimu.

“Vijana wanaweza kuwa faida au sumu kwa taifa … kama kijana atakosa elimu akaishia kukaa vijiweni ni rahisi kurubuniwa na kuingia katika vitendo viovu.

“Angalia maandamano mengi asilimia 90 ya washiriki ni vijana tena walioshia darasa la saba,” alisema Juma.

Wakati huohuo, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwatta) siku chache zilizopita lilikutanisha viongozi mbalimbali wa dini mkoani hapa kujadili misingi muhimu ya kufuata kwa ajili ya kulinda amani ya nchi.

Katika Kongamano hilo, Sheikh Mohamed Iddi, aliwasilisha misingi 10 ambako suala la elimu sahihi kwa vijana liligusiwa kama moja ya misingi muhimu ya kuhakikisha migogoro isiyo na tija haitokei. mingine ni jamii kujengwa katika misingi ya kumjua Mungu, siasa safi, uadilifu wa viongozi, kuheshimiana katika suala la dini, kuthaminiana, kuvumiliana, utii kwa uongozi uliopo, wanahabari kuheshimu taaluma yao na kutobaguana katika shughuli za jamii.

Chanzo;Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa