
Wanawake 12 ambao ni wazazi wa wasichana 21
waliofanyiwa ukeketaji wilayani Same, mkoa wa Kilimanjaro, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Same, wakati
waliposomewa mashitaka yao kwa mara ya kwanza tangu wakamatwe mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Watuhumiwa wote wanashitakiwa kwa kosa la Ukatili dhidi ya watoto na kuwasababisha maumivu makali, shitaka ambalo wote wamekana.
Miongoni mwa washitakiwa, mmoja alikabiliwa na
mashitaka mawili, moja akiwa mzazi wa mmoja wa wasichana waliokeketwa na
pia akiwa ngariba.
Kutokana na mila na desturi ya baadhi ya
makabila nchini, ukeketaji unafanyika japo ni kinyume cha
sheria, huku watu wanaokamatwa kuhusika na ukeketaji wakichukuliwa hatua
za kisheria.
Kama watapatikana na hatia, wanawake hao wanakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka mitano jela au kutozwa faini kubwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 30 Desemba 2013, wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.
Chanzo;Edwin mushi blog
0 comments:
Post a Comment