Home » » Mrema aanza jitihada kutoa TLP ‘ICU’ Vunjo

Mrema aanza jitihada kutoa TLP ‘ICU’ Vunjo

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro, kimepata pigo baada ya wanachama wake 28 akiwamo Mwenyekiti wa Kijiji cha Komalangoye, Israel Mtui na viongozi wengine saba kujiunga na Chama cha Tanzania Labour (TLP).

Licha ya mwenyekiti huyo wa chama, wamo Katibu wa CCM wa kijiji hicho, Thomas Matemu, Katibu wa vijana, Jofrey Minja, Mwenyekiti wa vijana, Sabas Minja na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Felister Matemu.
Wengine ni Paul Alex ambaye ni Balozi wa CCM Kitongoji cha Ikunda, Balozi wa Kitongoji cha Majengo, Estak Minja, Mwenyekiti wa CCM Kitongoji cha Liwari, Baltazari Minja, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Masoi Aqulin Kombe na Grace Mamiro Mwenyekiti Kitongoji cha Kiala chini ambao wote kwa pamoja walisema wamechoshwa na sera zisizotekelezeka za CCM.
Akiwapokea Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema hiyo ni filimbi kwa CCM kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Alisema chama kipo imara kamwe hawapo tayari kuendelea kukaa na chama kisichowaletea maendeleo.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa