MWANAMKE
aliyefahamika kwa jina la Bi. Aretas Joseph (48), mkazi wa Kijiji cha
Lesoroma, Tarafa ya Usseri, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro,
anatuhumiwa kufanya mapenzi na watoto wadogo wa kiume wenye umri kati ya
miaka tisa hadi 14.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa
Polisi mkoani humo, Robert Boaz, alisema Bi. Joseph alikamatwa Januari 8
mwaka huu, kutokana na ushirikiano uliotolewa na majirani zake.
Alisema
vitendo hivyo amekuwa akivifanya muda mrefu ambapo majirani waliweka
mtego na kufanikiwa kumkuta chumbani kwake akiwa na watoto watatu
wanaume akifanya nao mapenzi.
Aliongeza kuwa, baada ya fumanizi
hilo, majirani hao walitoa taarifa polisi ndipo mama huyo alikamatwa na
kufikishwa katika Kituo cha Polisi Rombo.
"Hawa watoto baada ya
kuhojiwa walisema wapo wanne na siku hiyo mwenzao hakuwepo...walisema
huyu mama huwa anawachezea sehemu zao za siri, kuwapaka mafuta na
kuwashawishi wafanye mapenzi kwa zamu.
" Uchunguzi wa awali wa polisi
unaonesha huyu mwanamke amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana
mmoja aliyekuwa amemaliza darasa la saba miaka mitano iliyopita na
kujaliwa kuzaa naye mtoto mmoja," alisema .
Hata hivyo, Kamanda Boaz
alisema baada ya Idara ya Ustawi wa Jamii kupata taarifa ya uhusiano
huo, ilifuatilia na hatimaye kukatisha uhusiano huo.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment