Home » » HATARI: MWANAMKE AUWAWA KIKATILI NA MPENZI WAKE KWA KUKATAA KUTOA PENZI

HATARI: MWANAMKE AUWAWA KIKATILI NA MPENZI WAKE KWA KUKATAA KUTOA PENZI

Jeneza la Marehemu, Sekunda Mushi (42), aliyeuwawa kinyama usiku wa kuamkia, Januari 6, wakiwa na majonzi katika mazishi ya mwanamke huyo anayedaiwa kuuwa kwa sababu ya kimapenzi baada ya kuibuka kwa ugomvi kati yake na Mpenzi wake, aliyetajwa kwa jina la Gerald Mamkwe.
Jeneza la mwili wa Marehemu Sekunda Mushi likiingizwa kaburini katika maziko yaliyofanyika jana katika kijiji cha Longuo A, kata ya Uru Kusini, manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Baba mzazi wa Sekunda Mushi (mwenye suti Nyuesi), akisikliza mahubiri ya mwisho katika ibada ya maziko ya mwanae, Sekunda Mushi, aliyeuwawa kikatili usiku wa kuamkia Januari 6 katika kile kile kinachodaiwa kuwa ni ugomvi wa kimapenzi.
Mzee Onesmo Mushi, ambaye ni Baba Mzazi wa Marehemu Sekunda Mushi, akiweka udongo katika kaburi la mwanamke huyo aliyeuwawa kinyama na mtu anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, kutokana na ugomvi wa kimapenzi.
Mama Aurea Mushi, ambaye ni Mama Mzazi wa Marehemu Sekunda Mushi, akiweka udongo katika kaburi la mwanamke huyo aliyeuwawa kinyama na mtu anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, kutokana na ugomvi wa kimapenzi.
 Picha Ziadi Bofya hapa KIJIWE CHETU BLOG

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa