Home » » COCAINE KILO 4 ZAKAMATWA SIKU YA DAWA ZA KULEVYA

COCAINE KILO 4 ZAKAMATWA SIKU YA DAWA ZA KULEVYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Cocaine kilo 4 zakamatwa Siku ya Dawa za KulevyaPOLISI mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kunasa dawa za kulevya zinazodaiwa kuwa ni Cocaine zenye uzito wa zaidi ya kilo nne, huku mhusika wa dawa hizo akiwatoroka polisi wa Kitengo cha Dawa za Kulevya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) katika mazingira tatanishi.
Tukio hilo linatokea wakati dunia leo inaadhimisha siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya ambayo huadhimishwa Juni 26 kila mwaka ambapo kitaifa yanafanyika jijini Mbeya yakibeba kaulimbiu ya “Uteja wa dawa za kulevya unauzulika na kutibika, chukua hatua”.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mkoani hapa, dawa hizo zikiwa zimefichwa kwa ustadi mkubwa ndani ya mikoba inayotumiwa na wanawake pamoja na mifuko ya kutunzia faili, zilikamatwa Juni 23, saa 10 alfajiri, katika Uwanja wa KIA.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Robert Boaz, alithibitisha kukamatwa kwa dawa hizo huku akisema hadi sasa bado hazijafahamika ni aina gani ingawa uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa ni Cocaine.
“Dawa hizi zilikuwa zimefichwa kwenye mabegi mawili makubwa ambayo ndani yake kulikuwa na pochi zinazotumiwa na wanawake, mhusika alionekana kana kwamba anafanya biashara ya mikoba kumbe katikati ya pochi hizo ndiko alikuwa ameficha,” alisema Boaz.
Alisema mzigo huo ulikamatwa uwanjani hapo ukidaiwa kuwa ni wa abiria aliyesafiri na  ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airline) iliyokuwa ikitokea Brazil na kupitia katika Uwanja wa Ndege wa  Addis Ababa, Ethiopia, kisha Mombasa na hatimaye kutua KIA.
Alisema abiria huyo ambaye majina yake yamefahamika pamoja na picha zake, anadaiwa kutelekeza mizigo yake uwanjani hapo na kukimbia mikono ya polisi huku akiomba kutozungumzia kutoweka kwake pamoja na kutotaja majina ya mhusika kutokana na sababu za kiupelelezi.
Chanzo;Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa