Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHUGHULI
za uchorongaji miamba katika machimbo ya moramu ya Longoma, Kijiji cha
Masaera, Kata ya Kilema Kusini wilayani Moshi Vijijini mkoani
Kilimanjaro, zimesitishwa kwa muda usiojulikana baada ya wachimbaji
wawili kuangukiwa na kifusi na kufariki dunia.
Tukio hilo limetokea kukiwa na kumbukumbu ya watu saba kupoteza maisha katika machimbo kama hayo ya Pumuani wilayani humo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika kijiji hicho, tukio hilo
lililotokea juzi majira ya saa 8 mchana, wakati vijana hao; Adrian
Blessing na Shukuru Temu, wanaokadiriwa kuwa na miaka kati ya 18 na 25,
walipoingia kwa kificho katika eneo ambalo lilizuiliwa kufanyika
shughuli za uchongaji wa tofali.
Diwani wa Kata ya Kilema Kusini, Kawawa Rudega, alisema tayari
serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Ibrahimu Msengi,
aliyekuwepo eneo la tukio juzi, imetangaza kusitisha shughuli za
uchimbaji katika machimbo hayo kwa muda usiojulikana.
“Mkuu wa Wilaya alikuwepo hapa jana (juzi), na aliagiza kusitishwa
kwa shughuli za uchongaji wa tofali katika eneo hilo na aliwaagiza
Mawakala wa Madini (TMAA), Kanda ya Kaskazini kufika katika eneo hili
kwa ajili ya kufanya tathmini ya kina kuhusu usalama wa machimbo hayo,”
alisema Rudega.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Husiwajali Kidaya, alisema vijana hao
walifikwa na mauti baada ya kukaidi amri ya mmoja wa viongozi wa
machimbo hayo, ya kuwataka kutoingia baada ya eneo kubwa kuanza kuweka
ufa.
“Ni juzi tu Jumamosi, mwenyekiti wa wachimbaji katika machimbo haya
alitoa agizo kwa vijana hawa kutoingia humu ndani, kutokana na hili gema
lililokatika kuonekana kuwa na ufa, walikaidi na kuingia jana kwa
kuibia kwa kujua haikuwa ni siku ya kazi,” alisema Kidaya.
Alisema baada ya kupokea taarifa za tukio hilo, alihamasisha wananchi
ambao walifika na kuanza zoezi la uokoaji wakiongozwa na timu nzima ya
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment