Home » » MVIWATA: ELIMU DUNI HUPOTEZA CHAKULA

MVIWATA: ELIMU DUNI HUPOTEZA CHAKULA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

ELIMU duni kwa wakulima imeelezwa kuwa chanzo cha upotevu wa chakula kuanzia hatua ya uvunaji, usafrishaji, ukaushaji, uchambuaji na maadalizi hadi kuhifadhi kwenye maghala ya chakula.
Hayo yamo kwenye taarifa ya utafiti uliofanywa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima nchini (Mviwata) mkoani Kilimanjaro, uliolenga kuibua changamoto zinazowakabili wakulima hapa nchini.
Utafiti huo unafanywa chini ya ufadhili wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya, ukizihusisha nchi za Uganda, Kenya na Tanzania ukilenga katika ushirikishwaji wa wakulima katika kuibua masuala yahusuyo usalama wa chakula.
Mratibu wa Mviwata mkoa wa Kilimanjaro, Alex Urio, alisema kuwa, utafiti umebaini kwamba wakulima wengi wana elimu ya darasa la saba ambapo asilima 82.5 ya waliohojiwa katika wilaya ya Hai, wana elimu ya msingi.
Chanzo:Tanzania daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa