Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama,
amezishauri kampuni za simu za mkononi kuhakikisha inawekeza katika
mtandao wa elimu ili kuwarahisishia wanafunzi wa vyuo katika sekta ya
elimu na kuboresha huduma zake kwa wateja.
Gama alitoa rai hiyo alipozindua Duka jipya la Tigo mjini Moshi jana.
Alisema ili kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inakua kila uchao, ni
lazima kuhakikisha kuwa wanazidi kuboresha huduma zake kwa wateja
ikiwamo kuwekeza katika sekta ya elimu.
Alisema katika kuhakikisha elimu inakua kwa kasi na kufanya
ushindani mkubwa katika soko la ajira za Afrika Mashariki, kampuni za
simu zihakikishe zinatoa fursa kwa wanafunzi kupata masuala mengi zaidi
kwa ajili ya kuleta mabadiliko.
“Tigo ni moja ya kampuni za simu ambazo zimekuwa zikikua kwa kasi
kubwa hapa nchini na kusababisha ushindani mkubwa na mitandao mingine.
Sasa imefika wakati kampuni hii kuangalia upya uwezekano wa kuwekeza
katika sekta ya elimu ili kuwanufaisha wanafunzi na wanavyuo wote katika
kuhakikisha kuwa wanapata kiurahisi huduma ya kielimu,” alisema Gama.
Awali, akisoma risala kwa Mkuu wa Mkoa, Meneja wa Ubora wa Huduma
kwa Wateja wa Tigo, Mwangaza Matotola, alisema duka hilo jipya
limefunguliwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa linawaondolea usumbufu
wateja wa mtandao huo ambao walikuwa wakisubiri huduma kwa muda mrefu
katika duka moja la mjini Moshi.
Matotola alisema uzinduzi wa duka hilo umefanyika ikiwa ni siku
moja baada ya kampuni hiyo kufungua duka lingine lililokarabatiwa jijini
Arusha, lengo likiwa ni kuboresha na kusogeza huduma karibu zaidi na
wateja wake.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment