………………………………………..
KITUO cha utafiti wa mazao kanda
ya kaskazini,SELIANI kimedhamiria kuwainua wakulima wa zao la
maharage kutokana na kuhamasisha wakulima kulima kilimo hicho kwa
kutumia mbegu bora za maharage zinazozaa sana ambazo zimefanyiwa
utafiti ambazo zitasambazwa kwa mawakala wa pembejo za kilimo mapema
Septemba mwaka huu.
Utafiti huo unatoa msukumo mpya
wa kuzalisha zao hilo kwa wingi na hivyo kuinua kipato cha mkulima
ambapo atapata mavuno mengi tofauti na aliyokuwa akiyapata kutokana na
kutumia mbegu ambazo hazijatafitiwa.
Mratibu, wa mradi huo,Eunice
Zakayo,ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akiwaelezea wakulima wa
kijiji cha Mlangoni, wilayani Siha,manufaa yatakayotokana
na utekelezaji wa mradi huo wa kilimo cha mazao ya mbegu bora za
maharage zilizofanyiwa utafiti na kituo cha kilimo cha Seliani pamoja na
mifuko maalumu ya kuhifadhia mazao,PICS.
Alisema ili kuhakikisha mkulima
ananufaika na utafiti huo, kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo,cha
Seliani,kituo hicho kinatekeleza mradi ambao utaongeza mavuno kwa
wakulima wanatumia mbegu bora za zao la maharage ambazo zimefanyiwa
utafiti na zinazaa sana .
Eunice ,ambae pia ni afisa
kilimo mtafiti mkuu alisema mradi huo unalenga kuwawezesha wakulima
kulima kilimo cha kibiashara ambapo hekari moja ina uwezo wa kuzalisha
magunia kati ya 10 hadi 15 tofauti na awali ambapo wakulima walikuwa
wakivuna magunia mawili kwa hekari. .
Eunice, amesema utafiti huo wa
mbegu bora za maharage unakusudia kuhamasisha wakulima kupanda mbegu
bora za maharage zilizofanyiwa utafiti zinazaa sana hazishambuliwi na
wadudu, magonjwa na haziathiriwi na hali ya hewa
Eunice , alisema kuwa mradi huo
unaenda sambamba na matumizi ya mifuko ya PICS ambayo ni maalumu
imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya
maharage kutoka shambani mifuko ambayo inayakinga na kuyalinda maharage
yasipekechwe na wadudu baada ya kuvunwa kwa kipindi cha miaka mitatu na
kuendelea .
Alisema mifuko hiyo mipya licha
ya kuwa ni mkombozi kwa mkulima pia ni kifaa bora cha kuhifadhia mazao
hivyo wakulima hawatakuwa na sababu ya kuendelea kutumi mitungi na
magudulia kuhifadhia mazao yao sanjari na matumizi ya dawa za kuulia
wadudu wanaopekecha mazao yakiwa ghalani.
Eunice, alisema mifuko hiyo ya
PICS, ambayo itakuwa ikipatikana kwa mawakala wa mbegu na pembejeo za
kilimo tu ili kuepuka kuchakachuliwa na wafanyabiashara .
Alisema mradi unawajali
wakulima wa zao la maharage ili wasipate hasara itakayotokana kwa
kuhifadhi mazao yao kwa kutumia vifaa duni ambavyo vinaruhusu wadudu
kuingia na kuishi kupekechua maharage na kuwapatia hasara wakulima.
Alisema kuwa lengo la mradi huo
ni kumuinua mkulimana ili apate mafanikio na kila mtaalamu wa kilimo
kwenye eneo husika atakuwa na shamba darasa ili kutoa elimu ya vitendo
kwa wakulima kuhusu kilimo cha mbegu bora za maharage ambzo zimefanyiwa
utafiti ili waweze kuongeza mavuno.
0 comments:
Post a Comment