Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgeni
rasmi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya
Afya na Usitawi wa Jamii akiwahutubia Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi
wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015
wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo
Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akielezea umuhimu
wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015
wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo
Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi
wa Sensa na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu akitoa maelezo ya awali wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo
ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Baadhi
ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na
Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakifuatilia kwa makini hotuba
ya mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo
iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mgeni
rasmi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya
Afya na Usitawi wa Jamii (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi
na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 mara baada ya kufunga mafunzo
ya utafiti huo wilayani Moshi, Kilimanjaro.
(PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).
NA: VERONICA KAZIMOTO.
Wito
umetolewa kwa viongozi wote wa Serikali katika Ngazi zote na wananchi
kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa
Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria utakaoanza rasmi tarehe 21
Agosti, 2015.
Wito
huo uletolewa leo na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii Dkt. Ahmed Makuwani wakati wa hafla fupi ya kufunga
mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika wilayani Moshi, Kilimanjaro.
"Ninawaomba
Wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi, Wasimamizi na
Wahariri watakaoshiriki zoezi la kukusanya Takwimu za Utafiti wa Afya ya
Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ili kupata taarifa muhimu na
sahihi kwa ajili ya kupanga Mipango na Sera endelevu za Sekta ya Afya
katika nchi yetu, amesema Makuwani".
Dkt.
Makuwani amesema kuwa taarifa zitakazokusanywa kwa wananchi kwa ajili
ya utafiti huo zitakuwa ni siri na zitatumika kwa shughuli za Kitakwimu
tu na wala hazina uhusiano wowote na Uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
kwa
upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina
Chuwa amesema utafiti huu wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka
2015 unalenga kukusanya taarifa nyingi za sekta ya afya zinazotumika
katika kutathmini malengo mbalimbali na pia kusaidia katika kupanga
mikakati mipya.
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu kwa mara nyingine tena inafanya Utafiti wa Afya ya
Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ambao kwa mara ya mwisho
ulifanyika mwaka 2010. Utafiti huu utaanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015
kwa nchi nzima na utamalizika mwishoni mwa Mwezi Februari 2016.
0 comments:
Post a Comment