Home » » MREMA AMFAGILIA DK MAGUFULI KUWA RAIS WA TANZANIA‏

MREMA AMFAGILIA DK MAGUFULI KUWA RAIS WA TANZANIA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), ambaye pia ni Mgombea ubunge Jimbo la Vunjo,  Augustino Mrema aliposimama kwa mudakuwasalimia wananchi Njia Panda ya Himo, mkoani Kilimanjaro. Mrema alimpigia debe Dk Magufuli kwa kuwataka watanzania wampigie kura nyingi za ndiyo ili awe rais PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli  akiwa na furaha wakati Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), ambaye pia ni Mgombea ubunge Jimbo la Vunjo,  Augustino Mrema akimuombea kura kwa wananchi aliposimama kwa muda kuwasalimia wananchi Njia Panda ya Himo, mkoani Kilimanjaro
 Mrema akitoa heshima baada ya kumuona Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli eneo la Njia ya Panda ya Himo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwa na  Mgombea ubunge Jimbo la Vunjo kupitia CCM, Innocent Shirima  wakiwapungia mikono wananchi walipokuwa wakiwasili kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Polisi wa Himo, Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro
 Wananchi wa Rombo wakimshangilia Dk Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni mjini Tarakea, Rombo
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Rombo, Samora mjini Tarakea
 Wananchi wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli alipowasili kwenye Uwanja wa Polisi Mjini Himo, Jimbo la Vunjo
 Dk Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni mjini Vunjo ambapo ameaomba wananchi kumpigia kura ili awafanyie kazi
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Vunjo, Innocent Shirima mjini Himo
Mgombea ubunge Jimbo la Vunjo kupitia CCM, Innocent Shirima, akikana mbele ya wananchi na Dk Magufuli uvumi uliozagaa kwamba anataka kuihama CCM kwenda Ukawa wakati wa mkutano wa kampeni katika mji wa Himo.
Dk Magufuli akionesha kadi ya mwanachama wa NCCR Mageuzi aliyeamua kuhamia ccm katika mkutano ulioffanyika mjini Himo, JImbo la Vunjo.
Wananchi wa Njia Panda ya Himo, Jimbo la Himo,wakishangilia baada kumuona Dk Magufuli. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


Wafanyabishara ndogondogo wanaofanya biashara kando kando ya barabara jimbo la Vunjo  wakaishangilia baada ya kuwaeleza viongozi wa serikali kuacha kuwatoza ushuru.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo akiwaelekeza wananchi jinsi ya kuipigia kura CCM,  ambayo katika karatasi la kupigia kura ipo nafasi ya tatu.
Wnanchi wwilayani Mwanga wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni mjini Mwanga
Wananchi wakisikiliza wakati Dk Magufuli akihutubia mjini Mwanga
Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Mwanga kupitia CCM, Profesa Jumanne Maghembe
Wananchi wa Kisiwani Jimbo la  Same Mashariki wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli
Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango katika mkutano uliofanyika  Ndungu
Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akitoa ahadi mbalimbali katika mkutano uliofanyika katika Mji wa Ndungu, Same Mashariki PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG..
Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Anne Kilango
Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akijinadi kwao mjini Same
Moja ya vionjo katika mkutano wa kampeni mjini Same
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Same. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa