Home »
» WATUMISHI WANNE HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI,WASIMAMISHWA KAZI NI BAADA YA KUKWAPUA ZAIDI YA MILIONI 70.
WATUMISHI WANNE HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI,WASIMAMISHWA KAZI NI BAADA YA KUKWAPUA ZAIDI YA MILIONI 70.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
|
Mkuu wa Wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na wananchi alipofanya ziara katika hosptali teule ya Machame na kuzungumza na wafanyakazi |
|
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame (hawapo pichani) . |
|
Baadhi ya iongozi wa Hosptali hiyo na viongozi wa serikali wa wilaya ya Hai. |
|
Wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame . |
|
Mkurugenzi wa Hosptali hiyo,Dkt Saitore Laizer akizungumza katika kikao hicho. |
|
Baadhi ya madktari wa hosptali teule ya Machame. |
|
Baadhi ya watumishi wa Hosptali hiyo. |
|
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi katika hosptali ya Machame ,Dkt Fredrick Muro akizungumza katika kikao hicho. |
|
Baadhi ya wafanyakazi. |
|
Mkuu wa wilaya akiondoka katika hosptali hyo mara baada ya kumalizika kwa kikao na watumishi .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
HALMASHAURI ya wilaya ya Hai,mkoani
Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake wanne kwa tuhuma za kughushi
hati za mishahara na kughushi nyaraka zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi
cha sh Mil 73.4 zikiwemo fedha za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari
na wauguzi wa Hospitali teule ya Machame.
Tuhuma hizo pia zina mtaja Mweka
hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri
hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha na kwamba tayari Uongozi wa hosptali hiyo iliyo
chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini ,umekwisha mfukuza kazi.
Watumishi wawili kati ya wanne
wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti,moja ni kughushi hati za
mishahara,vitambulisho na sahihi za watumishi
waliostaafu na wengine kuacha
kazi na kuchukua mikopo wa Mil 35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi
walioacha kazi.
|
0 comments:
Post a Comment