Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe akizungumza na Wadau wa
Utalii mkoa wa Kilimanjaro alipokutana nao katika ukumbi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Moshi.
Baadhi ya Wadau wa Utalii wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii (hayupo pichani) alipokutana nao.
Mhifadhi
Mkuu mpya wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita
Loibooki akiwa katika kikao hicho ambapo alitamburishwa rasmi akichukua
nafasi ya Erastus Lufunguro aliyehamishiwa Makao Makuu, Mhifadhi
Loibooki alikuwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA).
Baadhi ya wamiliki wa kampuni za Utalii wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Amosi Makala akizungumza wakati wa kikao hicho.
Aliyekuwa
Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, (KINAPA) Eva
Mallya ambaye kwa sasa amehamishiwa Hifadhi ya Taifa ya Manyara akiteta
jambo na Mhifadhi mkuu mpya wa KINAPA,Betrita Loibooki.
Katibu
wa Chama cha Waongoza Watalii mkoa wa Kilimanjaro (KGA) James
Mong'ateko akiwasilisha malalamiko ya wapagazi mbele ya Waziri wa
Maliasili na Utalii .(hayupo pichani)
Waziri
Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi
wakimsikiliza kwa makini katibu wa Chama cha Waongoza watalii mkoa wa
Kilimanjaro (KGA) James Mong'ateko (hayupo pichani ) alipokuwa akieleza
changamoto.
Mkurugenzi
Mkuu Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati
wa kikao cha Waziri wa Utalii na Wadauu wa Utalii kilichofanyika mkoani
Kilimanjaro.
Katibu
wa KGA,James Mong'ateko akikabidhi kwa Waziri Maghembe taarifa
iliyohusu Changamoto mbalimbali wanazopata katika shughuli za kupanda
Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya Wadau wa Utalii katika kikao hicho.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
0 comments:
Post a Comment