Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akimtwika maji mama
katika Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi mara baada ya kuzindua mradi wa
maji kijijini hapo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA),
Inj. Ruth Koya akimuonyesha Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj.
Gerson Lwenge moja ya miradi ya maji inayotekelezwa na mamlaka hiyo,
Kata ya Moshono, Wilayani Arumeru.
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akizungumza mbele ya Waziri wa
Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, viongozi na wananchi wa Longuo,
Wilayani Moshi.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na Mkuu wa Wilaya
ya Moshi, Novatus Makunga (kulia) na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na viongozi na
wataalamu aliombatana nao kwenye ziara yake kwenye chanzo cha maji cha
Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji cha Bangata,
kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru
…………………………………………
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge amezindua mradi wa maji
wa Longuo, katika Kijiji cha Longuo, Wilaya ya Moshi mwishoni mwa wiki
katika ziara yake mkoani Kilimanjaro. Mradi huo unaohudumia vijiji vya
Longuo na Kariwa, umekuwa faraja kubwa kwa wananchi, ambao kwa muda
mrefu walikuwa na tatizo la kupata huduma ya majisafi na salama na
kusababisha hatari ya magonjwa ya milipuko kwa wananchi.
Mhe.
Lwenge, amefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua siku
themanini tu kukamilika, na kuipongeza Mamlaka ya Majisafi na Mazingira
Moshi (MUWSA) kwa usimamizi mzuri wa mradi huo. Pia, alitembelea chanzo
cha maji, chemchemi ya Kisimeni iliyopo Kata ya Uru Kusini ambayo
inachangia uzalishaji wa maji katika Wilaya ya Moshi.
Vilevile,
Mhe. Lwenge alitembelea miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA). Katika ziara yake hiyo
mkoani Arusha, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, aliweza kufika kwenye
chanzo cha maji cha Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji
cha Bangata, kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru ambao
unachangia asilimia ishirini ya uzalishaji maji kwa Jiji la Arusha.
Pia,
alifika kwenye chanzo cha maji cha chemchemi ya Machare, iliyopo Kata ya
Moshono, Wilayani Arumeru iliyovamiwa na wananchi wanaofanya shughuli
za kibinadamu kinyume na sheria na kuhatarisha uzalishaji wa maji ya
kutosha kwa ajili ya kuhudumia mji wa Arusha.
0 comments:
Post a Comment