Mwenyekiti wa TLP taifa Dkt. Augustino Lyatonga
Mrema amesisistiza ombi lake la kazi kwa kumkumbusha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwamba ampe kazi yoyote
amsaidie kibarua kigumu alichonacho cha kuwahudumia watanzania.
Dkt. Mrema ameyasema hayo alipokuwa akizungumza
na EATV kuhusu miaka 32 ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania
Edward Moringe Sokoine ambaye alihudumu kwenye awamu ya kwanza ya Mwl.
Julius Nyerere ambapo alifariki akiwa na cheo cha waziri mkuu tarehe
12.04.1984 kwa ajali ya gari.
''Namkumbuka Sokoine kama mtu wa watu
aliyehudumia watu aliyepambana na ufisadi na magendo alikuwa anatenda
haki kwa wananchi wote hata mimi nilipokuwa waziri wa mambo wa ndani na
naibu waziri mkuu nilijaribu kufanya kama yeye bahati mbaya sikufanikiwa
kama yeye kwa sababu sikuwa waziri mkuu au Rais''- Amesisistiza Mrema.
Kuhusu Mrema kuomba kazi kwa Dkt. Magufuli
Mrema amesema kwa kutambua rekodi yake ya utendaji kazi Rais Dkt.
Magufuli aliwahimiza wananchi wa Vunjo wamchague kipindi cha kampeni na
yeye akampigia kampeni na Rais akawaambia wananchi wa Vunjo kwamba Mrema
akikosa ubunge atapangiwa kazi nyingine ndiyo hiyo wananchi wanaulizia.
Aidha Mrema amesema kuna maeneo ambayo yeye
anafiti siyo lazima apewe madaraka makubwa mimi sihitaji ukuu wa mkoa au
uwaziri anipe kazi yoyote na nikionana naye nitamkonyeza maeneo ambayo
ninafiti ili nimsaidie kutumbua majipu.
Hata hivyo Dkt. Mrema amempongeza Dkt. Magufuli
kwamba ni mtendaji ambaye ameamua bila kusukumwa kupambana na mafisadi
na kwamba yeye ni alfa na omega na kazi hiyo ameonyesha kwamba atafanya
vizuri kuliko Sokoine na Mrema.
0 comments:
Post a Comment