Katibu
Mkuu akiwa anatoa msaada katika shule ya watoto wenye ulemavu wa akili
na viungo katika shule ya msingi mreyai iliyoko ndani ya wilaya ya
rombo.
Shaka akiwa anapanda MTI katika shule ya watoto wenye ulemavu mreyai rombo
Shaka akiwa na baadhi ya wanafunzi
Na Woinde Shizza, Rombo
Viongozi
wa kisiasa, wafanyabiashara, viongozi wa kiserikali na wafanyajazi
wametakiwa kuwajali na kuwathamini sana watoto wenye ulemavu na
wanaoishi kwenye mazingira magumu kwani wao pia ni binadamu wanao
sitahili kupata haki na mahitajj muhimu ya kibinadsmu
Hayo
yamebainishwa leo na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka
wakati alipotembelea shule ya msingi Mreyai iliyopo wilayani Rombo
mkoani Kilimanjaro yenye huduma ya watoto wenye ulemavu wa viungo na
Mtindio wa akili.
Alisema
kuwa ni muhimu kuwajali sana watoto wenye ulemavu kwani wakitengenezwa
vizuri na kuandaliwa vizuri kwa kupewa elimu watakuwa viongozi wazuri
wa baadae.
Aidha
alivitaka vyama Vya siasa vijielekeze kutatua changamoto na ma tatizo ya
watoto ambao ni Walemavu na sio kuendeleza Kufanya siasa hata sehemu
ambayo haitakiwi siasa.
"Napenda
kuviambia vyama vingine vya siasa, sasa hivi uchaguzi umeisha, ni
kipindi cha kufanya kazi na kuachana na mambo ya siasa, sasa hivi ni
kipindi cha kufanya kazi na kutatua matatizo ya wananchi " alisema
Shaka.
Kwa
upande wa Mkuu wa shule ya msingi Mreyai, Nuruel Laizer alisema kuwa
shule hiyo inahudumia wanafunzi wenye Mtindio wa akili na wanafunzi
ambao ni walemavu wa viungo,amesema kuwa shule hiyo inakabiriwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa chakula cha wanafunzi,
ukosefu wa vitanda na mgodoro ya kulalia Wanafunzi ambao ni walemavu
,baiskeli kwa ajili ya watoto ambao ni walemavu wa miguu.
Alisema
kuwa Wanafunzi hao wanakaa katika mabweni hapo shuleni, lakini
wanaupungufu mkubwa wa vitanda na mgodoro, kwani vitanda ambavyo wana
vitumia wameviazima kutoka kwa watu na mda wowote wenyewe wanaweza kuja
kuvichukuwa.
Aliomba
serekali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia ili watoto
hao waweze kuishi kwa amani na furaha kama watoto wengine."watoto hawa
wana wazazi lakini wazazi hao hawana uwezo na ndio maana wamewaleta hapa
ili wapate elimu, hivyo tunaomba sana serekali na wadau mbalimbali
wajitokeze kutusaidia"alisema laizer
Shule
hii ya msingi Mreyai imepata msaada wa chakula, maharage, malindi,
sabuni, mafuta, miswaki na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu
Shaka aliaidi kusaidia shule hii vitanda Nane na mgodoro kwa ajili ya
wanafunzi hawa wenye ulemavu wa viungo pamoja na Mtindio wa ubongo.
0 comments:
Post a Comment