Home » » JESHI LA POLISI KILIMANJARO LAWATUNUKU ZAWADI ASAKARI WAKE 34.

JESHI LA POLISI KILIMANJARO LAWATUNUKU ZAWADI ASAKARI WAKE 34.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akipokea salamu za heshima kutoka kwa askari wakati wa gwaride maalum lililoandaliwa wakati wa hafla fupi ya kutunuku zawadi kwa askari 34 wa vyeo mbalimbali waliotekeleza vyema majukumu yao.kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Wilbroad Mutafungwa.</ div >
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akikagua gwaride la heshima baada ya kuwasili katika viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia mjini Moshi kwa ajili ya hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akihitimisha ukaguzi wakati wa gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza asakari walitekeleza vyema majukumu yao.
Gwaride likitoka kwa mwendo wa haraka mara baada ya kumalizika kwa ukaguzi.
Ofisa Mnadhimu wa jeshi la Polisi  mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 wa jeshi hilo waliotekeleza vyema majukumu yao.
Baadhi ya maofisa wa jeshi la Polisi wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa askari 34  waliotekeleza vyema majukumu yao.
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuoneesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq baadhi ya silaha zilizokamatwa hivi karibuni zikidaiwa kutumika katika vitendo vya uharifu.
Mkuu wa Kitengo cha dawa za kulevya cha jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Mkaguzi wa Polisi,Ezekiel Midala akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro sehemu ya dawa za kulevya zilizokamatwa na jeshi hilo.
Baadhi ya askari waliotunukuwa zawadi kwa utendaji kazi mzuri wakisonga mbele kwa ajili ya kutunukiwa zawadi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akitunuku zawadi kwa baadhi ya askari waliofanya vizuri katika kutekeleza majukumu yao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Asante Tours ,Cuthbert Swai akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutoa zawadi kwa asakari waliofanya vizuri wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Pikipiki mbili aina ya Fekon zilizotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Asante Tours ,Cuthbert Swai kusaidia jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akiwa ameketi juu ya pikipiki na kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Mwandamizi Msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutoa zawadi kwa askari  34 wa jeshi hilo mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akitoa cheti kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo akitambua mchango wa wadau kwa jeshi la Polisi. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa