WATANZANIA
WAASWA KUPUNGUZA POMBE ILI WACHAPE KAZI
Frank
Mvungi- MAELEZO
Watanzania
wameaswa kupunguza unywaji wa pombe ili waweze kushiriki katika ujenzi wa
uchumi wa viwanda na kulifikisha taifa kwenye uchumi wa kati ifikapo 2020.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele kutoka Wizara
ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Prof. Ayoub Maghimba amesema
kuwa ni vyema watu wakapunguza unywaji wa Pombe ili kutumia muda mwingi katika
uzalishaji na kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
“Magonjwa
yasiyo ya kuambukiza ni pamoja na
Saratani,magonjwa ya moyo,magonjwa sugu ya njia ya hewa,seli
mundu,magonjwa ya akili na dawa za kulevya,magonjwa ya figo,kisukari,ajali, na
magonjwa ya macho yasiyo ya kuambukiza” Alisisitiza Prof. Maghimba.
Akifafanua
Prof. Maghimba alisema kuwa utafiti uliofanyika ulionyesha asilimia 15.9 ya
wananchi wanavuta sigara, asilimia 29.3 wanakunywa pombe, asilimia 97.2
wanakula mbogamboga na matunda chini ya mara tano kwa siku hali inayowaweka
katika hatari ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Alisema kuwa
unywaji wa pombe uliokithiri unasababisha magonjwa kama saratani ambayo
inachangia vifo na wastani wa wagonjwa 109 hugundulika na saratani kila siku hapa
nchini.
“Magonjwa
yasiyo ya kuambukiza au magonjwa sugu ni magonjwa ambayo mtu akiyapata hawezi
kuambukiza wengine na ataishi nayo hadi siku ya kufa.” Alisisitiza Prof.Maghimba.
Magonjwa
haya yamekuwa yakiongezeka duniani kote, hasa kwenye nchi zilizo chini ya
Jangwa la Sahara,Tanzania ikiwemo. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanachangia
asilimia 27 ya vifo vyote duniani.
0 comments:
Post a Comment