Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi wa mkoa wa
Kilimanjaro katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa
yaliyofanyika mkoani humo
Wananchi wakimsikiliza
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa
yaliyofanyika mkoani humo, leo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama
Barabarani na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta
ya Ujenzi), Mhandisi Joyce Mbunju, akieleza mikakati inayofanywa na Serikali
katika kudhibiti ajali za barabarnia kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipotembelea Banda la Wizara hiyo
katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa
yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro
Mpima magari kutoka mzani wa Himo, mkoani
Kilimanjaro kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo Mhandisi Adam
Labay, akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipotembelea Banda la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama
Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kwenye maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa
Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiungana na kikundi
cha ngoma za asili cha Msanja, kutoka Mkoani Kilimanjaro kucheza ngoma hiyo katika maadhimisho ya Wiki ya
nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani humo, leo.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.
Madereva wa Pikipiki
(bodaboda) nchini wametakiwa kutii sheria za Usalama Barabarani bila shuruti kwani
ajali nyingi zinazotokea barabarani zimekuwa zikisababishwa na uzembe unaofanywa
na madereva hao.
Akizungumza leo katika
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama kitaifa mkoani Kilimanjaro Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,
amesema kuwa chanzo kikuu cha ajali hizo ni uharaka walionao madereva hao na
ukosefu wa mafunzo ya usalama barabarani kwa baadhi ya madereva.
“Madereva wa bodaboda
naomba mbadilike, muwe na tabia ya kutii sharia za usalama barabarani bila
shuruti kwani ajali nyingi nchini zimekuwa zikisababishwa na nyinyi kutokana na
haraka haraka zenu”, amesema Makamu Rais.
Aidha, amefafanua kuwa
Tathmini iliyofanywa na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani kuanzia
mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu katika mkoa wa Kilimanjaro imebaini kuwa
kuna ajali za Pikipiki 84 zilizojitokeza ambazo kati ya hizo, 61 zimesababisha
vifo na zilizobaki majeruhi.
Kuhusu ajali za mabasi
ya abiria Mheshimiwa Makamu wa Rais amesema kuwa zimepungua kutokana na uwepo
wa mbinu za udhibiti wa mabasi hayo kama vile upigaji picha kwa magari
yanayozidisha spidi yakiwa barabarani (Tochi), na ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa na
Jeshi la polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani katika magari ya abiria
nchini.
Makamu wa Rais
amefurahishwa na mkakati wa Serikali wa uandaaji wa mfumo mpya na wa kisasa wa
kuweka kamera zitakazorekodi makosa ya usalama barabarani yanayofanywa na
madereva nchini.
Ametoa rai kwa Askari
wa Usalama Barabarani kutotumia kigezo cha kupiga Tochi kwa kuwaonea,
kuwanyanyasa madereva na kudai rushwa kwani vitendo havikubaliki kisheria na
hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo.
“Taswira tunayoitaka
ni kuwa wananchi wawaone askari kama
walinzi wa mali zao na maisha yao na si vinginevyo”, amesisitiza Makamu wa
Rais.
Katika hatua nyingine,
Makamu wa Rais amelitka Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na wadau wake
kuhakikisha wanabadilisha mbinu za namna ya kukabiliana na tatizo la ajali
nchini na kuongeza nguvu katika kudhibiti mwendo kasi, ulevi kwa madereva,
kutovaa kofia ngumu kwa waendesha bodaboda, kutofunga mkanda kwa baadhi ya
abiria na ukosefu wa vifaa vya kuwalinda watoto wadogo wakiwa kwenye gari.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba (Mb), amemhakikishia Makamu
wa Rais kuwa wataboresha na kuunda mbinu mbalimbali ili kudhibiti ajali za
barabarani zinazoweza kuepukika.
Amewataka wananchi
kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kupunguza ajali za
Barabarani na kuwasisitiza madereva kuzingatia sheria za usalama Barabarani
kwani hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote anayekiuka sheria hizo.
Naye, Makamu
Mwenyekiti wa Baraza hilo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa (Mb), amesema
kuwa Baraza limekuwa likifanya jitihada mbalimbali ili kudhibiti ajali za
barabarani kama utoaji wa elimu kwa umma kupitia vyombo vya Habari kama
Televisheni na Redio pamoja na uandaaji wa viperushi na majarida.
Maadhimisho ya Wiki ya
nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa yaliyobeba kauli mbiu “Zuia ajali, Tii
Sheria – Okoa maisha”, kwa mwaka huu yameadhimishwa mkoani Kilimanjaro amabapo
yameshirikisha wadau mbalimbali wa usalama nchini.
0 comments:
Post a Comment