Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua kiwanda
kidogo cha uzalishaji wa kahawa katika Bodi ya Kahawa mara baada ya
kuwasili Ofisi hizo kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua namna Kahawa inavyohifadhiwa tayari kwa kuingia sokoni.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisikiliza maelezo
ya kitaalamu kuhusu mchakato mzima wa kupaki kahawa na soko lake kutoka
kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa kahawa na uhamasishaji
masoko.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe alipotembelea chumba
cha kuchotea Sampuli zinazopelekwa ambazo ni kilo 8 na kuchotea Gramu
300 kwa Loti.
Muonjaji katika Maabara ya Kahawa Bi Regina Mushi Daud akiendelea na majukumu yake katika maabara ya Kahawa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa kahawa na uhamasishaji masoko Kutoka Bodi ya Kahawa akielezea mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe namna wanunuzi wanavyokabiliana katika ununuzi wa Kahawa
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizungumza na
wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazo
Baadhi
ya wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa wakifatilia kikao kilichoongozwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe katika
Ukumbi wa Bodi hiyo.
Picha ya pamoja wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe.
Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameitaka Bodi ya
Kahawa ambayo ni Taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la kusimamia sekta
ya Kahawa nchini kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa Kahawa nchini
kwani Kahawa ni miongoni mwa mazao ya kipaumbele.
Mhandisi
Mtigumwe ametoa Rai hiyo wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Bodi ya
Kahawa Mara baada ya kutembelea Ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mtaa wa
Railway, Kata ya Mawenzi Katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Alisema
kuwa Mwaka 2011 wadau waliandaa na kupitisha mkakati wa miaka 10 wa
maendeleo ya Kahawa ambayo lengo kuu ilikuwa ni kuongeza uzalishaji hadi
kufikia Tani 80,000 Mwaka 2017 na Tani 100,000 Mwaka 2021 lengo ambalo
halijafikia na bado uzalishaji ni mdogo hivyo kuongeza uzalishaji
linapaswa kuwa jambo la haraka iwezekanavyo.
Katibu
Mkuu Alimuelekeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa Kahawa na
uhamasishaji Masoko Kufanya Utafiti ili kubaini nini chanzo cha
uzalishaji mdogo wa Kahawa iwapo wananchi kutotunza vizuri kahawa yao,
Hali ya hewa na udongo au mbegu sio nzuri zinazotumika.
Aliongeza
kwa kusema kuwa Serikali inajipanga kwa kampeni kubwa kutoa elimu kwa
wananchi juu ya kufahamu umuhimu wa kulima kwa wingi mazao ya Chakula na
Biashara ikiwemo zao la Kahawa.
Hata
hivyo Katibu Mkuu huyo, Alisema miongoni mwa sababu ambazo huchangia
uzalishaji mdogo katika mazao mbalimbali nchini huwa ni pamoja na
Wananchi kuchanganya mazao wakati wa kupanda jambo ambalo sio rafiki
sana katika Kilimo, sambamba na Kutoacha nafasi kati ya mche na mche.
Mhandisi
Mtigumwe aliitaka Bodi ya Kahawa Kufanya Utafiti wa maeneo ambayo Kahawa
inastawi kwa wingi ili kuongeza sehemu za kuzalisha Kahawa kufikia
uzalishaji wa kiwango kikubwa tofauti na ilivyo hivi sasa.
Hata
hivyo amesema kuwa atazishughulikia haraka iwezekanavyo Changamoto za
Uzalishaji, Changamoto za Ubora, Changamoto za Masoko sambamba na
Changamoto za Sekta.
Majukumu
ya Bodi ya Kahawa ni pamoja na usimamizi wa sheria namba 23 ya
marekebisho yake ya Mwaka 2009 na kanuni za Kahawa 2013 sambamba na
kuratibu Majukumu shirikishi (Shared Functions) Baina ya serikali na
wadau.
0 comments:
Post a Comment