MKOA wa Klimanjaro, umepongezwa kwa
kuitikia agizo la Rais John Magufuli la kutaka kila mkoa ubainishe fursa
za uwekezaji zilizopo na kuandaa mwongozo wa uwekezaji.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda katika hafla ya uzinduzi wa
mwongozo wa uwekezaji mkoa wa Kilimanjaro uliondaliwa na Taasisi ya
Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Akimwakilisha Waziri wa Nchi wa Ofisi
hiyo Selemani Jafo, Naibu Waziri huyo alisema kwamba agizo la Rais
ambalo limelenga kuweka mikakati mahsusi ya kuipeleka nchi katika uchumi
wa viwanda.
Akitoa salamu za pongezi kwa Mkuu wa
mkoa, Mh. Anna Mghwira Naibu Waziri Kakunda alisema wakati mkoa wa
Kilimanjaro unatekeleza maagizo, serikali kuu nayo inaendelea kuboresha
mazingira ya kufanyia biashara ili kuvutia wawekezaji mbalimbali.
- Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mh. Joseph Kakunda akitoa hotuba wakati wa kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro kwa niaba ya Waziri wa Nchi wa Ofisi hiyo, Mh. Selemani Jafo (hayupo pichani) kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa jengo la NSSF mjini Moshi, mkoani humo.
Akizungumzia Mwongozo huo Naibu Waziri
alisema kwamba kazi ya kubaini fursa za uwekezaji katika miradi
mbalimbali yenye faida siyo tu kwa wawekezaji pekee bali pia kwa taifa
letu kupitia kodi na upatikanaji wa bidhaa na huduma mbalimbali kwa kila
eneo la nchi.
Alisema kazi iliyofanywa na mkoa huo ina
maana kubwa kwa kuwa sasa inakuwa rahisi kwa wawekezaji wawe wa ndani au
nje kujua namna ya kuwekeza katika mkoa wa Kilimnjaro kwa kuzingatia
mahitaji yao na namna rasilimali watu na miundombinu ilivyo.
Alisema agizo la Rais la utengenezaji wa
mwongozo unakwenda sanjari na ubainishaji na uandazi wa maeneo ya
uwekezaji ili yanapotakiwa yapatikane hima.
- Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mh. Joseph Kakunda (katikati) kutoa hotuba ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo uliondaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour.
Aliutaka mkoa huo kuutangaza mwongozo wao
kwani biashara ni matangazo katika maeneo mbalimbali ya kimataifa na ya
wawekezaji katika masoko ya hisa kwa njia ya kielektroniki ili wavune
utayari wao wa kukaribisha uwekezaji.
Kakunda alisema kwamba mkoa huo kwa asili
unaweza kabisa kuvutia wawekezaji. Kinachostahili kufanywa kwa sasa ni
kuhakikisha kauli mbiu ya Kilimanjaro ya Viwanda, inawezekana chukua
hatua inatekelezwa kwa vitendo.
Akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna
Mghwira alisema kwamba Mwongozo huo utafanyiwa kazi na matunda yake
yataonekana wakati taifa linaelekea kwenye uchumi wa viwanda.
Alisema mkoa huo una rasilimali za kutosha kuwezesha wawekezaji
mbalimbali kutekeleza adhma ya kuwa na viwanda vidogo na vya kati
vinavyotumia rasilimali kutoka mkoani.
Aliwashukuru wataalam wa ESRF waliwezesha kupatikana kwa muongozo huo na wafadhili ambao ni UNDP.
Naye Dk Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi
Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ambayo ndiyo
ilipewa jukumu na Mkoa wa Kilimanjaro kufanya utafiti na uchambuzi wa
kina ili kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa, aliupongeza
mkoa wa Kilimanjaro kwa kuona umuhimu wa kuwa na mwongozo wa uwekezaji.
Aidha katika hotuba yake hiyo alisema
kuwa taasisi yake ilitengeneza sehemu tatu za taarifa ambazo zote
zililenga kutoa uwanda mpana kwa wawekezaji kuwa na taarifa muhimu za
uwekezaji katika mkoa wa Kilimanjaro.
- Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Mbaga Kida akitoa taarifa kuhusu uandaaji wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na taasisi yake kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) katika hafla iliyofanyika mjini Moshi kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF.
Alisema katika hotuba yake kwamba ESRF
ilifanikiwa kuandaa ripoti tatu ambazo ni Ripoti ya Fursafiche katika
Viwanda (Industrialization Potentials Report), Ripoti ya Fursa za
Uwekezaji (Investment Opportunities Report) pamoja na Mwongozo wa
Uwekezaji ambao Mkoa umezindua rasmi leo.
Pia alisema kwamba Ripoti hizo
zilithibitishwa na Mkoa Oktoba 12, 2017 katika warsha maalum
iliyoandaliwa na Mkoa wa Kilimanjaro.
Mapema mwaka huu Mwongozo kama huo ulizinduliwa Mkoani Simiyu ambao umeleta matokeo makubwa ndani ya muda mfupi. Wiki
mbili zilizopita mkoa wa Mwanza nao ulizindua mwongozo wa uwekezaji.
Mkoa wa Mara katika siku za usoni unatarajiwa kuzindua mwongozo wa
uwekezaji. Miongozo yote hiyo imeandaliwa na ESRF.
Alisema miongozo hiyo ya Uwekezaji
inaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Mpango wa Pili wa Taifa
wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016 – 2021) unaosisitiza ujenzi wa
Tanzania ya Viwanda ili kuifikisha nchi katika uchumi wa kati ifikapo
2025.
Katika hotuba yake pia Dk Kida
aliiushukuru Uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Mkuu wa Mkoa, Anna
E. Mghwira, Katibu Tawala wa Mkoa, Mhandisi Aisha S. Amour na viongozi
wengine wa mkoa na wilaya zote kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa
wataalamu wakati wanapita kutafuta maoni.
Aidha alitoa shukurani kwa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa ufadhili wa fedha.
- Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa nne kulia), Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (wa tatu kushoto), Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira (wa nne kushoto), Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (wa tatu kulia) Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF Bi. Margareth Nzuki (wa pili kulia), Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dkt. Hoseana Lunogelo (kulia), Watafiti vijana kutoka ESRF Bw. Mussa Martine (kushoto) pamoja na Bw. Joseph Nyampepela Ngonyani (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiwa wameshika nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Pia alishukuru timu ya ESRF ikiongozwa na
Bi. Margareth Nzuki, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu kwa kuratibu,
watafiti washiriki Prof. Haidari Amani; Dkt. Hoseana Lunogelo na Prof.
Samuel Wangwe kwa kupitia mwongozo huu.
Aidha aliwashukuru watafiti vijana Bw.
Mussa Martine, Bw. Joseph Nyampepela Ngonyani pamoja na Bw. John
Shilinde. Aidha, alisema anatambua mchango mkubwa aliotoa marehemu
Abdallah Hassan katika uandaaji wa Mwongozo huu.
Pia alisema ESRF ipo kwa ajili ya
maendeleo ya nchi na wananchi wake na hivyo wasisite kuwatumia pale
wanapohitaji msaada wa kitaalam.
- Mshiriki Mtafiti wa ESRF, Dkt Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji mkoani Kilimanjaro zilizoonekana wakati wa kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mwongozo huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua rasmi Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro huku Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto), Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira (wa pili kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (kulia) wakishuhudia tukio hilo katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akionyesha nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuzindua rasmi huku Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto), Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira (wa pili kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (kulia) wakishuhudia tukio hilo katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akikabidhi nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa Mkuu wa mkoa huo, Mh. Anna Mghwira (wa pili kushoto) mara baada ya kuzindua rasmi huku Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) amoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (kulia) wakishuhudia tukio hilo katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Mbaga Kida akipeana mkono na Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi wakati wa kukabidhi nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Kilimanjaro na wadau wa maendeleo Ubalozi wa Uholanzi na taasisi zingine huku wakiwa wameshika nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo baada ya kuzinduliwa rasmi.
0 comments:
Post a Comment