na Asha Ban
WIZARA ya Maliasili na Utalii imesema suala la utoroshwaji wa wanyamapori kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) kwa sasa linashughulikiwa na mamlaka nyingine za serikali na kwamba liko mahakamani.
Taarifa kwa vyombo iliyosainiwa na Msemaji wa wizara hiyo, George Matiku, ilieleza wamekuwa wakipata maswali mengi kutoka kwa waandishi wa habari na watu binafsi wakihitaji kujua ripoti na undani wa suala hilo, jambo ambalo liko nje ya uwezo wao.
Taarifa hiyo ilieleza wizara kwa sasa haina wajibu wa kulitolea taarifa na kwamba taarifa ya kamati iliyoundwa na Katibu Mkuu ni kwa matumizi ya ndani ya wizara na si ya kusambazwa kwenye vyombo vya habari au kwa mtu mwingine yeyote.
“Kamati iliundwa na taarifa imekabidhiwa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii na kwamba inaendelea kufanyiwa kazi hivyo kuna haja ya kukaa kimya kusubiri utendaji utakaofanyika,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Mwaka jana Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliunda kamati ya wabunge wanne kuchunguza utoroshwaji wa wanyamapori hai, wakiwamo twiga wawili.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment