Home » » UNAMATUMAINI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO MWAKA HUU?

UNAMATUMAINI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO MWAKA HUU?


Kilimanjaro
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani kutokana na mandhari nzuri ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote Afrika na inapatikana katika nchi ya Tanzania.
Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini. Kilele cha Kibo chenye urefu wa mita 5895 (futi 19340) ndio kivutio kikubwa kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na kufunikwa na theruji.
Mlima huu ni moja kati ya milima ambayo kilele chake hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka kila pande za dunia.
Safari ya kupanda mlima huu humpitisha mpandaji katika kanda za hali ya hewa tofauti kuanzia ile ya nchi za tropiti hadi arktiki.
Zaidi ya watalii 20,000 hupanda mlima huu kila mwaka wakiwemo wageni kutoka nje ya nchi na Watanzania. Mpandaji wa mlima huu huhitaji angalau siku tano, siku tatu kupanda na siku mbili kuteremka.
Kuna njia sita ya kupanda mlima Kilimanjaro hadi kileleni.Njia iliyo rahisi na maarufu zaidi ni ile ya kuanzia lango la Marangu, ambako ndiyo makao makuu ya hifadhi.
Wanyama kadhaa hupatikana katika msitu unaozunguka Mlima Kilimanjaro wakiwemo mbega, nyani, nyati, chui, tembo, swala na ndege.

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi

Kuanzai mwezi Disemba hadi februari, na pia mwezi Julai na Septemba (ingawa wakati huu ni baridi zaidi)
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa