Home » » Waethiopita, Wasomali 42 mbaroni Kilimanjaro

Waethiopita, Wasomali 42 mbaroni Kilimanjaro


na Charles Ndagulla, Moshi
WIMBI la wahamiaji haramu wanaoingia nchini kupitia njia za panya linazidi kushamili kila uchao ambapo juzi mkoani Kilimanjaro polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni raia 39 wa Ethiopia na Wasomali watatu wakiwa ndani ya nyumba moja.
Kukamatwa kwao kulifuatia taarifa zilizotolewa kwa jeshi la polisi na raia wema juu ya kuwapo kwa wahamiaji hao haramu kwenye nyumba hiyo wakiwa njiani kusafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini kupitia mikoa ya nyanda za juu kusini.
Wahamiaji hao haramu wenye umri kati ya miaka 18-32 wamekamatwa ikiwa ni wiki moja tangu kuokotwa kwa maiti 45 za raia wa Ethiopia kichakani katika kijiji cha Chitego wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma na wengine 84 wakiwa hai.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, ilieleza kuwa wahamiaji hao walikutwa katika nyumba moja katika kijiji cha Kilototoni wilaya ya Moshi Vijijini.
Hata hivyo polisi hawajataja jina la mwenye nyumba walimokutwa wahamiaji hao zaidi ya kusema jina lake halijafahamika mara moja na kwamba wahamiaji hao watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya taratibu za kisheria kukamilika.
Wakati polisi wakisita kutaja jina la mwenye nyumba, uchunguzi wa TanzaniaDaima umebaini kuwa wahamiaji hao walivuka mpaka na kuingia nchini Juni 30 kupitia kijiji cha Madarasani kilichoko upande wa Kenya
Chanzo: Tanzania Daima


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa