na Charles Ndagulla, Moshi
RAIA wa Tanzania na Wanigeria wawili, wanashikiliwa na vyombo vya dola nchini Malaysia, wakituhumiwa kukutwa na kete za dawa za kulevya wakijiandaa kuzisafirisha kwenda nchi ambayo hadi sasa haijatajwa.
Habari zilizoifikia TanzaniaDaima mwishoni mwa wiki, zimemtaja Mtanzania huyo kuwa ni Carlos Vicent Mmasi mkazi wa jijini Arusha huku majina mawili ya raia wa Nigeria yakiwa bado hayajajulikana.
Akithibitisha kukamatwa kwake, baba mzazi wa Carlos, Vicent Mmasi, alisema kuwa mwanaye tayari ameshafikishwa mahakamani nchini humo akikabiliwa na mashtaka ya kupatikana na dawa za kulevya.
Hata hivyo, Mmasi ambaye ni mfanyabiashara anayejihusisha na uuzaji wa magari jijini Arusha, alimtetea mwanaye akidai kuwa hahusiki na tuhuma hizo na kwamba Wanigeria aliokamatwa nao ndiyo waliokuwa na mzigo huo .
Bila kufafanua kazi anayofanya mwanaye huko malaysia, Mmasi alisema siku ya tukio ambayo hata hivyo hakuitaja, mwanaye alikuwa akiendesha gari na raia hao wa Nigeria walimuomba lifti na hakuelewa walichokuwa wamebeba.
Kwamba mwanaye alijikuta akisimamishwa na polisi na baada ya kupekuliwa ndipo ilipobainika kuwa ndani ya gari lao kulikuwamo na dawa za kulevya.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment