Home » » POLISI MOSHI WAKAMATA GARI LILILOIBIWA TANESCO DAR

POLISI MOSHI WAKAMATA GARI LILILOIBIWA TANESCO DAR

Enos Masanja, Moshi
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kukamata magari matatu yanayosadikiwa kuibwa katika maeno mbalimbali nchini likiwemo moja
linalomilikiwa na makao makuu ya shirika la umeme nchini Tanesco

Gari hilo  aina ya toyota land cuicer lenye nambari za usajili SU 38739 lilikamatwa katika nyumba  ya mkazi mmoja wa kijiji cha Machame - Nronga  wilayani Haialiyetambulika kwa jina la Tumsifu Werakiko Lema .
Maafisa wa polisi walifanikiwa kukamata gari hilo lililoibwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupata msaada wa vifaa kutoka kampuni ya Car Track yenye kujihusisha na ufungaji wa vifaa malumu vya kudhibiti wizi kwenye magari.
Kamanda wa polisi mkoani kilimanjaro Bwana Robert Boaz amewaambia waandishi wa habari kuwa jeshi lake lilifanikiwa kulikamata gari hilo jumanne jioni nyumbani kwa tumsifuni likiwa tayari limebadilishwa namba na kuwekwa namba za bandia na baada ya upekuzi lilifanikiwa kukamatamagari mengine mawili ambayo yanasadikiwa kuibwa mahali kusikojulikana.

Mtuhumiwa wa wizi huo ameripotiwa kuwaponyoka polisi kwani alitoweka muda mfupi baada ya kubaini kuwa nyumba yake imezingirwa   na jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kushirikiana nalo ili aweze kukamatwa.

Mkoa wa Kilimanjaro umekuwa ukishuhudia vitendo kadhaa vya wizi wa magari na duru za kiintelijensia zinadokeza kuwa magari mengi yanayoibwa huuzwa nchi jirani za Kenya na Uganda huku baadhi yake
yakitenganishwa na kuuzwa kama vipuri hapa nchini

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa