Home » » SABA WAKAMATWA KWA KUHARIBU SENSA

SABA WAKAMATWA KWA KUHARIBU SENSA

na Rodrick Mushi, Moshi
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama amesema kuwa, kuna vikundi vya watu wachache wa dini ya Kiislamu vinavyowashawishi watu wasihesabiwe katika mkoa huo.
Gama alieleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kueleza kuwa, kukiwa kumebakia siku moja kabla ya kuanza kwa kazi hiyo, Vikundi hivyo vipo kwenye Wilaya za Same, Mwanga, Moshi na Hai, ambapo hadi sasa watu saba ndio waliokamatwa.
Alisema kutokana na hali hiyo alilazimika kufanya mikutano kwenye wilaya ambazo tatizo hilo lilionekana kuwa kubwa ili kuwahamasisha wananchi.
Alielezea changamoto nyingine iliyopo katika Wilaya ya Hai kuwa ni wenyeviti wa vitongoji kugomea kuwapokea wageni ambao ni makarani wa sensa kwa ajili ya kuwatembeza kwenye maeneo yao ya kuhesabu watu.
Pia mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa, alikwishapokea malalamiko kwa wenyeviti wa vitongoji 116 ambao wanadai serikali posho zao tangu 2009 hadi mwaka jana.
“Ni kweli nilipokea barua kutoka wenyeviti hao wa vitongoji,lakin maamuzi yao yalikuwa ni ya pamoja,hivyo uamuzi wa wao kama watahudhuria au hawatahudhuria itajulikana leo na nilitaka nipate barua ya mmoja mmoja,” alisema Gama.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa