Home » » WANANCHI WERUWERU WATAKIWA KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO

WANANCHI WERUWERU WATAKIWA KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO

Na Omary Mlekwa, Hai
DIWANI wa Kata ya Machame Weruweru, Adris Mandrai, amewataka wananchi kujituma kuchangia miradi ya maendeleo katika meneo yao.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mijongweni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, alisema ushirikiano wa wananchi katika kuchangia miradi inayotekelezwa na Serikali utasaidia kufikisha huduma kwa jamii kwa wakati.

Aidha, amewaagiza viongozi wa vijiji na kata kusimamia miradi ya maendeleo sanjari na kudai stakabadhi zinazoonyesha kiasi cha fedha zinazotumika katika miradi inayoanza kutekelezwa katika maeneo yao.

“Kusuasua katika mchango huo wa ujenzi wa shule kumesababishwa na baadhi ya wananchi kutothamini suala zima la elimu ambalo ni hatari katika kuinua kiwango cha taaluma,” alisema Mandrai.

Awali, aliwataka wananchi wa kata hiyo kuhakikisha wanaunga jitihada za Serikali ya wilaya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mnepo, kila mwananchi alitakiwa kuchangia Sh 5,000, ambapo halmashauri hiyo imeidhinisha Sh milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.

Alisema pamoja na jitihada za Serikali, pia aliyekuwa Mbunge wa Hai, Fuya Kimbita, aliwahi kuchangia Sh milioni tano kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo.

Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa