Home » » TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 LAZINDULIWA KWA KISHINDO MJINI MOSHI

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 LAZINDULIWA KWA KISHINDO MJINI MOSHIMkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mh Leonidas Gama akimtaja mshindi aliyejinyakulia gari aina ya Vits iliyokuwa ikinadiwa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,maara baada ya kuchezeshwa droo usiku huu,pichani mwanzo kulia ni Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru,Muwakilishi kutoka michezo ya bahati nasibu ya Taifa,Abdallah Mohamed akishuhudia tukio hilo,na mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini,Mh Dr Msengi wakishuhudia tukio hilo usiku huu ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Leonidas Gama sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini, Mh Dr Msengia wakiingia kwa shangwe kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 usiku huu kwa ajili ya kulizindua tamasha hilo ambalo limepokelewa vyema kwa wakazi wa mji huo na vitongoji vyake. Pichani kulia ni Dj Zero akikamua vilivyo.
Dj Pq kutoka Clouds FM akikamua vilivyo kwenye mashine,kati ni mtangazaji wa Clouds FM B Dozen na mdau mwingine wakifuatilia kwa makini makamuzi yanayoendelea usiku huu,ambapo washabiki kibao wamejitokeza ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika.
Pichani shoto ni msanii kutoka THT,Recho sambamba na wacheza shoo wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Moja ya kikundi mahiri  kutoka THT kkikionesha mbwembwe zake jukwaani.
Dj Zero akikamua vilivyo.
Moja ya kikundi cha  THT kikiwa katika picha ya pamoja.
Picha zaidi ingia hapa chini

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa