Home » » KINAPA YAKAMATA NG’OMBE 150 HIFADHINI

KINAPA YAKAMATA NG’OMBE 150 HIFADHINI


Mwandishi wetu, Moshi-Kilimanjaro Yetu 
Jumla ya ng’ombe 150 wamekamatwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) wakidaiwa kuingizwa kwa lengo la kutafutiwa malisho jambo ambalo limekuwa likichangia uharibifu wa mazingira.
Kukamatwa kwa mifugo hiyo kumetokana na operation maalumu inayoendeshwa na askari wa hifadhi hiyo ikiwa ni jitihada za kuunusuru mlima Kilimanjaro ulioko katika hatari ya kutoweka kutokana na theluji yake kuyeyuka kwa kasi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro bwana Leonidas Gama aliyezuru katika makao makuu ya hifadhi hiyo yaliyopo marangu wilayani moshi ameonya wananchi wanaoendelea kufanya uharibifu katika mlima huo.
Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo Bwana Erastus Lufungulo ameiomba idara ya mahakama kuharakisha usikilizwaji wa kesi inayohusu mifugo hiyo kutokana na ugumu uliopo kuwahudumia ng’ombe waliokamatwa.
Kwa karibu miezi sita sasa, serikali katika mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na uongozi wa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro imekuwa katika harakati za kurejesha uoto wa asili katika mlima huo mrefu kuliko yote barani afrika.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa