WANANCHI wametakiwa kujenga tabia ya kutoa taarifa mbalimbali zinazohusiana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo yao na kuachana na hofu juu ya usalama wa maisha yao ili kukabiliana na vitendo hivyo.
Ushauri huo umetolewa na Mwanasheria kutoka kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake (WLAC)Jane Salomo wakati wa ufuatiliaji wa kampeni ya tunaweza inayoendeshwa na hicho kwa kushirikiana na kituo cha wasaidizi wa sheria mkoa wa Morogoro(MPLC)..
Solomo amesema kumekuwa na hofu kwa jamii juu ya utoaji wa taarifa za ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo kwa kuhofia usalama wao jambo ambalo linasababisha baadhi ya matukio yanayotokea katika maeneo mbalimbali kutoripotiwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kwa upande wake mkurugenzi wa MPLC, Flora Masoy amesema kuwa katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii ni jukumu la kila mmoja kutoa taarifa kwa vyombo husika ili kuweza kudhibiti tatizo hilo na kwamba vitendo vingi vya ukatili vimekuwa vikifanyika lakini haviripotiwi kutokana na sababu mbalimbali hivyo kuchangia athari mbalimbali ikiwemo kuvunjika kwa ndoa nama ongezeko la watoto wa mitaani.
Aidha wadau wengine wa masuala ya sheria, Regina Mahita na Levina Chuma toka toka manispaa ya Morogoro na wilaya ya Mvomero wamesema kuwa ukatili umekuwa ni mkubwa hasa kwa wanaume kuwafanyia vitendo vya ukatili wanawake wao huku baadhi yao wakishindwa kufahamu mahali pa kufikisha malalamiko yao huku wakibainisha katika kushughulia kukabiliana na vitendo hivyo wamejikuta wakijengewa chuki na baadhi ya vyombo vya sheria kutokana na wakati mwingine mazingira ya rushwa kujitokeza.
Naye Mwanasheria wa MPLC Clara Charwe alisema kupitia kampeni ya tunaweza wanalenga kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii na kwamba ukatili wa kijinsia umegawanywa katika makundi manne ikiwemo ukatili wa kiuchumi, Kingono, kisakolojia na kimwili huku vitendo vya watoto kushuhudia vitendo vya ukatili katika familia zao kumekuwa kukiwaathiri kisaikolojia kwa kuwajenga kuwa wakatili hata siku za baadaye.
0 comments:
Post a Comment