Na Florah Temba,
Moshi.
HALMASHAURI ya manispaa ya moshi Mkoani Kilimanjaro imeendesha zoezi la bomoabomoa nyumba za biashara na makazi ziliozojengwa kinyume cha sheria ili kuweka mji huo katika mpangilio ikiwa ni adhima ya kupanua mji wa moshi kuelekea jiji.
Operation hiyo imefanyika majira ya saa saba usiku katika kata mbalimbali za Manispaa hiyo ikiwemo Majengo,Pasua,Njoro na maeneo ya katikati ya mji.
Akizungumzia zoezi hilo mkurugenzi mtendaji wa manipsaa ya moshi Bi. Bernadette Kinabo, alisema hatua hiyo imetekelezwa baada ya kuzingatia taratibu za kisheria ikiwemo kuwaarifu watu waliojenga kinyume cha taratibu.
Alisema Halmashauri hiyo haitavifumbia macho vitendo vya uvunjaji wa sheria ikiwemo kujenga pasipokuzingatia sheria na taratibu za mipango miji kutokana na kwamba vitendo hivyo vinafifisha jitihada za manispaa hiyo za kutaka kupanua mji huo na kufikia jiji.
“Suala hili la kubomoa nyumba hizi,limezingatia taratibu zote kwani tulishatoa taarifa kwa wahusika na kuwataka wabomoe lakini hawakufanya hivyo,na tulitoa matangazo mengi ya kuendesha zoezi hili la kubomoa kwani zinafanya mji kuonekana kukosa mpangilio”alisema Bi. Kinabo.
Wakizungumza baadhi ya wakazi wa manispaa ya moshi waliofikwa na bomoabomoa hiyo wamelalamikia kitendo kilichofanywa na halamshauri ya manispaa ya Moshi na kusema kuwa kimewatia hasara kubwa.
Walisema manispaa hiyo haikuwataarifu kuhusiana na suala hilo ili waweze kuhamisha mali zao hali ambayo imewafanya kupata hasara kubwa kutokana na kwamba mali zao za bishara zimeharibika katika nyumba hizo.
Manispaa ya moshi iko katika mchakato wa kukamilisha taratibu za kisheria zitakazoiwezesha kuwa jiji.
0 comments:
Post a Comment