Home » » Tanzania na Kenya zatiliana sahihi mkataba wa kurahisisha biashara mipakani

Tanzania na Kenya zatiliana sahihi mkataba wa kurahisisha biashara mipakani




 Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samweli Sitta akizungumza na wananchi wa Kenya na Tanzania wakati wa mkutano uliofanyika Taveta nchini Kenya.
 Waziri Sitta akiwatambulisha wakuu wa wilaya Dk Ibrahim Msengi wa wilaya ya Moshi (kulia)  na Novatus Makunga wa wilaya ya Hai.
 Wananchi wa Tanzania na Kenya wakinyoosha mikono kuashiria kuruhusu kufanyiwa kazi kwa vigezo 12 vilivyo tiliwa saini na pande hizo mbili za Kenya na Tanzania.
 Waziri wa jumuiya ya Afrika mashariki nchini Tanzania Samweli Sitta na waziri wa jumuiya ya Afrika mashariki nchini Kenya Musa Sirma wakitia saini makubaliano 12 likiwemo la kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wa
mipakani mwa nchi hizo kuingia katika nchi nyingine kufanya biashara bila hati ya kusafiria na wakuu wa wilaya za mipakani wameagizwa kukaa pamoja na kuandaa utaratibu utakaotumika.
 Mawaziri wakibadilishana hati baada ya kutia sahihi
 Wakionesha hati kwa wananchi
Waziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kenya Musa Sirma(Kulia)akimkaribisha mgeni wake waziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samweli Sitta kuzungumza na wananchi wa Kenya na
Tanzania.
 Mawaziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kenya Musa Slima na wa Tanzania Samweli Sitta wakitoka kwenye ofisi ya DC Taveta kuhudhulia mkutano wa hadhara uliofanyika Taveta Kenya na kuhudhuliwa na wananchi
wa Tanzania na Kenya.
 Kikundi cha nyimbo cha nchini Kenya kikiongoza wimbo wa jumuiya ya Afrika mashariki.
Kikundi cha Ngoma cha Msanja cha mkoani Kilimanjaro kikitumbuiza wakati wa mkutano wa mawaziri wa jumuiya ya Afrika mashariki wa Kenya na Tanzania ulifanyika Taveta nchini Kenya.


Picha na Habari na Dixon Busagaga 
wa Globu ya Jamii, Moshi. 
Serikali za tanzania na kenya zimetangaza hatua kadhaa za kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wa mipakani mwa nchi hizo kuingia katika nchi nyingine kufanya biashara bila hati ya kusafiria na wakuu wa wilaya za mipakani wameagizwa kukaa pamoja na kuandaa utaratibu utakaotumika. 

 Makubaliano hayo yamefikiwa katika wilaya ya Taveta nchini kenya na kusainiwa na mawaziri wa jumuia ya afrika mashariki Bw Samwel Sita wa Tanzania na Musa Srima wa Kenya mbele ya wananchi wa pande zote hizo katika mkutano wa hadhara ambao viongozi hao walitoa ufafanuzi juu ya hatua hizo. 

 Waziri Sita amezitaja baadhi ya hatua hizo kuwa na fomu maalum za kuwatambulisha wafanyabiashara hao kufanya biashara zao katika masoko ya jirani yaliyo ndani ya umbali wa kilomita 20 kati ya nchi na nchi wakiwemo waendesha pikipiki. Akitoa ufafanuzi waziri Srima amesema, katika makubaliano hayo maafisa forodha wa pande zote wametakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa wafanyabiashara wakubwa ya namna uvushaji na ulipaji wa ushuru wa bidhaa zao na kuangalia uwezekano wa kufanya kazi kwa saa 24 wa idara zzote zikiwemo za uhamiaji.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa