na Rodrick Mushi, Hai
WANANCHI
wa Kijiji cha Kwa Sadala, wamemng’oa Mwenyekiti wao wa kijiji, Ernest Samwel,
baada ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.
Wananchi
hao walifikia uamuzi huo katika mkutano mkuu uliofanyika jana baada ya uongozi
uliokuwa umetoka wilayani kutaka kuahirisha mkutano huo.
Hali
hiyo ilisababisha mzozo na hatimaye wananchi na uongizi Uongozi wa Wilaya
kupitia Katibu Tawala Mpotwa walikubaliana kupigwa kwa kura za kutokuwa na
imani na mwenyekiti huyo.
Katika
kura hizo, 154 zilimkataa mwenyekiti huyo huku kura 124 zikimtaka mwenyekiti
huyo aendelee kuwapo madarakani.
Diwani
wa Masama Kusini, Issa Kisanga, alisema miongoni mwa tuhuma zilizomuondoa
mwenyekiti huyo madarakani ni kuuza maeneo ya wazi kiholela, kuingiza kijiji
kwenye mgogoro na kanisa, kutoa lugha chafu kwenye mikutano ya hadhara, pamoja
na kutofanya mikutano ya kusoma mapato na matumizi.
Alisema
baada ya hatua hiyo kufikiwa kilichobaki ni wananchi kusubiri uongozi wa wilaya
kutangaza taratibu za kumpata mwenyekiti wa kijiji wa muda kwa ajili ya
kuongoza kijiji hicho huku kukisubiriwa kutangazwa kwa uchaguzi.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa kijiji hicho aliyevuliwa uongozi, Ernest Samwel
alipopewa nafasi ya kujibu tuhuma zinazomkabili, alipinga baadhi ya malalamiko
kama ya uuzaji wa maeneo huku akisema malalamiko mengine ni ya kupandikizwa.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment