Mwandishi
wetu, Hanang’
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amependekeza kuvunjwa kwa Taasisi za
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwani badala yake kupambananayo
inaipalilia.
Akfungua tawi ya Chadema Kata za Katesh linalopakana na ofisi za Takukuru
Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara juzi, Mbowe alisema taasisi hiyo imeshindwa
kazi.
Mbowe alisema Takukuru imeshindwa kudhibiti hata rushwa ya wazi ndani ya CCM
kwenye chaguzi ambazo zilifanyika hivi karibuni.
“Hakuna ambaye hakujua rushwa ndani na CCM na jinsi ambavyo imeathiri chama
hicho, lakini Takukuru wameshindwa kupambana na rushwa hiyo badala yake
wanailea,” alisema Mbowe.
Alisema Rais Jakaya Kikwete ambaye anasimamia Takukuru iliyopo kwenye wizara
yake, ameshindwa kuibana ndiyo sababu hata yeye amekuwa akilalamika.
Pia, Mbowe alifungua matawi kata za Endasaki na Ganana, alisema kutokana na
Takukuru kushindwa kupambana na rushwa, isipovunjwa chama hicho kikiingia
madarakani kitawatimua watendaji wote wa taasisi hiyo ili wafanye kazi
nyingine.
Alisema Takukuru imeshindwa hata kusaidia kurejesha mabilioni ya fedha za
Watanzania ambayo yamefishwa nchini Uswis.
“Hawa Takukuru walipaswa kuanza kufanya uchunguzi juu ya fedha hizo baada ya
kupata taarifa na kusaidia taifa kuzipata, lakini wamekaa kimya,” alisema
Mbowe.
Alisema kutokana na ukimya huo, ndiyo sababu Chadema kupitia Naibu Katibu Mkuu
wake, Kabwe Zitto waliomba serikali kufanya uchunguzi na kutoa taarifa bungeni
juu ya walioficha fedha na utaratibu wa kuzirejesha.
“Bunge lijalo, kama wasipoleta taarifa ya maana juu ya fedha za Uswis tunajua
la kufanya, nadhani mmeona jinsi hoja hii ilivyoungwa mkono na watu
wengi,”alisema Mbowe.
Awali, Mbowe alizitaka ofisi hizo za Chadema, alizofungua kuwa kimbilio la
wanyonge kutoa kero zao na kusaidiwa badala ya kuwa maeneo ya kukaa viongozi
pekee.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment