Home » » Uchafu wakithiri pembezoni mwa Moshi

Uchafu wakithiri pembezoni mwa Moshi

LICHA ya Mji wa Moshi kusifika kwa usafi, lakini Serikali mkoani Kilimanjaro imekiri uchafu umekithiri katika maeneo ya pembezoni na kuitaka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kuchukua hatua za makusudi kuudhibiti.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama.

Alisema hali bado ni mbaya katika maeneo ya pembezoni, jambo ambalo linazidi kushusha hadhi ya usafi katika halmashauri hiyo na inahatarisha usalama wa afya za wakazi wa mji huo.

Alisema mji wa Moshi umekuwa ukiongoza kwa usafi, lakini kwa sasa hali si nzuri kwa kuwa kumekuwa na uchafu wa kutisha katika maeneo mbalimbali ya mji huo, jambo ambalo linahatarisha afya za wakazi wa manispaa hiyo.

Aidha, alisema kampuni za usafi zinazo kabidhiwa dhamana ya kusimamia suala hilo, yamekuwa yakiwanyanyasa watu kwa kudai rushwa.

Alisema halmashauri hiyo haina budi kuwawajibisha kampuni hayo yanayochukua tenda hizo kwa kuwa wamekuwa wakifanya biashara na utapeli kwa wananchi, jambo ambalo linalalamikiwa mara kwa mara.


Chanzo : Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa